logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Marcelo Bielsa kuifunza timu ya taifa ya Uruguay

Mfukufunzi Marcelo Bielsa achukua atamu za ukufunzi katika timu ya Taifa ya Uruguay.

image
na Davis Ojiambo

Michezo12 May 2023 - 09:01

Muhtasari


  • • Bielsa amewai zifunza timu ya taifa ya Argentina, Chile, timu ya Atletico Bilbao, Marseille, Lille, Lazio na timu ya Leeds.
Meneja wa zamani wa timu ya Leeds.

Mfukufunzi wa zamani wa Leeds Marcelo Bielsa amechukuwa hatamu za ukufunzi katika timu ya Taifa ya Uruguay.

Mkufunzi huyo alipigwa kalamu baada ya msururu wa matokeo mabaya katika klabu ya Leeds kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

 Aidha meneja huyo ni moja wapo wa wakufunzi wanaoenziwa sana katika ulingo wa soka duniani na hata meneja wa timu ya Manchester City pep Guardiola amewai msifia akisema kuwa Bielsa ni mojawapo wa wakufunza bora duniani.

Bielsa, anatarajiwa kutia saini kandarasi ya mkataba wake utakao dumu hadi Kombe la Dunia 2026 huku Uruguay ikimwamini kwa mradi wao wa muda mrefu.

"Atajiunga nasi katika siku zijazo, hatimaye yote yamekubaliwa", mjumbe wa Shirikisho la soka nchini Uruguay Jorge Casales alithibitisha.

Mwanahabari tajika wa maswala ya uhamisho wa wanasoka Fabrizio Romano alitangaza haya katika akaunti yake ya Instagram.

Bielsa amewai zifunza timu ya taifa ya Argentina, Chile, timu ya Atletico Bilbao, Marseille, Lille, Lazio na timu ya Leeds.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved