logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rashford kusalia Man U muda mrefu baada ya kusaini mkataba mpya

Marcus Rashford anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na timu ya Epl Manchester United.

image
na Davis Ojiambo

Michezo17 July 2023 - 10:57

Muhtasari


  • • Marcus Rashford anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na timu ya Epl Manchester United baada ya kufikia makubaliano na klabu hiyo.
  • • Paris Saint-Germain walikuwa wakihusishwa pakubwa kuhusu kutaka kumnunua Rashford, hasa kwa kuzingatia uwezekano wa kumpoteza mchezaji nyota Kylian Mbappe.
Marcus Rashford kutia saini mkataba wa miaka mitano Manchester United.

Marcus Rashford anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na  Manchester United baada ya kufikia makubaliano na klabu hiyo ya Epl

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa lakini hivi karibuni ataweka wazi juu ya masharti mapya, ambayo huenda yakajumuisha ongezeko kubwa la mshahara wake wa £200,00 kwa wiki.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikataa mapendekezo ya  kusajiliwa kwa timu za Ligi ya Premia na vilabu vya nje na kupendelea kuendelea na taaluma yake katika kalbu ya United hadi 2028, ripoti ya Athletic ilidhihirisha.

Paris Saint-Germain walikuwa wakihusishwa pakubwa na Rashford, hasa kwa kuzingatia uwezekano wa kumpoteza mchezaji nyota Kylian Mbappe.

Mkufunzi wa mashetani wekundu Erik ten Hag, hata hivyo, alishikilia kuwa ana uhakika mchezaji huyo atafikia makubaliano na klabu yake ya utotoni kuhusu kandarasi mpya.

"Natarajia Marcus Rashford kufanya upya," Ten Hag aliiambia Viaplay mwezi Mei. "Anaitaka. Manchester United inaitaka. Yeye ni mtoto wa klabu hii, kwa hivyo nadhani hili litatokea."

Baada ya kucheza mechi yake ya kwanza mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 18, Rashford alimalizia msimu wa 2022/2023 na mabao 17 licha ya kuwa na jeraha mwanzoni mwa msimu huo.

Mhitimu huyo wa akademia ya United, ambaye alijiunga na vijana wa klabu hiyo alipokuwa na umri wa miaka saba, hivi majuzi alikanusha ripoti zinazodai kwamba alikuwa akidai pauni 500,000 kwa wiki ili kusaini mkataba mpya. "Kabla tu huyu hajaanza kufanya raundi! Ni upuuzi mtupu," Rashford aliandika kwenye Instagram.

Habari hizi sasa zinapokelewa kwa furaha tele kwa mashabiki wa Man United baada ya timu hiyo kukamilisha usajili wa Mason Mount kutoka kwa mahasibu wa wakubwa Chelsea huku wakielekea kukamilisha usajili wa mlinda lango Andre Onana kutoka Inter Milan.

Sajili hizi zinatarajia kuboresha kikosi cha Mholanzi Ten Hag ambaye aliisaidia klabu hiyo kumaliza ndani ya mabano ya nne bora katika ligi kuu nchini England na kujithibitishia nafasi yao katika ligi ya mabingwa bara Ulaya msimu 2023/2024.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved