- Waziri wa serikali Irene Montero alisema: "Ni aina ya unyanyasaji wa kijinsia ambao wanawake hupitia kila siku."
Rais wa shirikisho la soka la Uhispania Luis Rubiales amekosolewa kwa kumbusu midomo Jenni Hermoso baada ya Uhispania kushinda Kombe la Dunia la Wanawake.
Rubiales alimbusu Hermoso wakati wa hafla ya utambulisho kufuatia ushindi wa 1-0 wa Uhispania dhidi ya Uingereza kwenye fainali Jumapili.
"Sikupenda," Hermoso alisema kwenye Instagram, lakini taarifa iliyotolewa baadaye kwa niaba yake ilimtetea Rubiales.
Waziri wa serikali Irene Montero alisema: "Ni aina ya unyanyasaji wa kijinsia ambao wanawake hupitia kila siku."
Montero, waziri wa usawa wa Uhispania, aliongeza kuwa hadi sasa imekuwa "isiyoonekana" na kwamba ni kitu "hatuwezi kuhalalisha".
"Hatupaswi kudhani kwamba kumbusu mtu bila ridhaa ni kitu 'kinachotokea'," alisema.
Katika maoni yaliyotolewa baadaye na shirikisho la soka la Uhispania Hermoso - mfungaji bora wa muda wote wa Uhispania - alisema wakati huo ulikuwa "ishara ya asili ya mapenzi".
"Ilikuwa ni ishara ya hiari ya kuheshimiana kwa sababu ya furaha kubwa inayoletwa na kushinda Kombe la Dunia," mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliongeza.
Vitendo vya Rubiales vilishutumiwa vikali kwenye mitandao ya kijamii, akiambiwa jiuzulu sasa hivi 'dimision yani' - kwa Kiingereza - ikivuma kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, nchini Uhispania.
Rubiales aliliambia shirika la utangazaji la Uhispania COPE kwamba lilikuwa "busu kati ya marafiki wawili wakisherehekea jambo fulani" na wale walioliona kwa njia tofauti kama "wajinga na wajinga".
01