Mshikilizi wa rekodi ya Afrika wa mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala amepongeza serikali kwa ufhadhili inaotoa kwa wanariadha.
Mwanariadha huyo aliwapa matumaini wanariadha watarajiwa ambao wana ndoto ya kujiunga na mchezo huo kutia bidii.
"Tunapata furaha kutoka kwa serikali wakati tunapofanya vyema katika mashindano yetu licha ya kukumbwa na changamoto nyingi serikali yetu inafanya michezo yetu kuwa rahisi kwa kutupa fedha za kufanikisha mbio zetu kwa wakati ufaao",alisema.
Mwanariadha huyu pia aliwapa motisha wanariadha wengi ambao hawajafanikiwa katika michezo yao akiwataka kutokata tamaa na kuendelea kufanya bidii kila wakati ndiposa siku moja wapate kufurahia jasho lao.
Omanyala aliwataka wazazi na walezi kuwaunga mkono watoto wao katika kila wanachofanya, ili kuanza kukuza vipawa vyao mapema ndiposa wafanikiwe kwa maisha kupitia talanta zao mbalibali.
"Maisha sio rahisi watu wanatuona kwenye Runinga na kudhani tumefika huko kwa bahati lakini hatufiki huko kwa bahati nzuri ila tumejitahidi sana kufika huko, na tumekuwa na dhamira, uthabiti na uvumilivu kumfikisha mtu yeyote pale", alisema.