Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (“CAF”) leo limetangaza ongezeko la 40% la Pesa kwa Mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies (“AFCON”) litakalofanyika nchini Côte d'Ivoire kuanzia wiki ijayo katika Makala ya 2024.
Mshindi wa TotalEnergies AFCON Côte d'Ivoire 2024 atapokea dola za Kimarekani USD 7 000 000, sawa na shilingi za Kenya bilioni 1.2.
Mshindi wa Pili wa TotalEnergies AFCON Côte d'Ivoire 2024 sasa atapata USD 4 000 000, sawa na shilingi milioni 631.
Kila mmoja wa Washindi wawili wa Nusu Fainali atapata USD 2 500 000, sawa na shilingi milioni 394 na kila mmoja kati ya wanne waliofuzu Robo Fainali, USD 1,300,000.
Rais wa CAF Dk Patrice Motsepe alisema:
“CAF imepata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika kuongeza Pesa za AFCON na mashindano yake mengine yote makubwa. Tumeongeza Pesa ya Tuzo ya Mshindi wa AFCON hadi USD 7 000 000 ikiwa ni ongezeko la 40% kutoka Pesa ya awali ya Tuzo ya AFCON. Nina imani kuwa sehemu ya Pesa ya Tuzo itachangia katika kuendeleza soka na pia kuwanufaisha wadau wote wa soka, pamoja na kusaidia Vyama vyetu vya Wanachama katika tawala zao.”
Mashindano hayo yatazihusisha timu 24 na yatang’oa nanga mnamo Januari 13 hadi Februari 11 nchini Ivory Coast.