Mwanariadha mwenye mshikilizi wa rekodi kadhaa kwenye mbio za mita 100, Usain Bolt amevunja kimya kwa ujumbe wa hisia nzito ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipoibiwa Zaidi yabilioni mbili pesa za Kenya kutoka kwa akaunti yake ya benki.
Januari 11 mwaka jana, Bolt aligonga vichwa vya habari baada ya kudai kwamba alipokea ujumbe ukimwambia kwamba dola milioni 12.7 za Kimarekani zimetoweka kutoka kwa akaunti yake ya benki kwa njia za utata.
Nguli huyo wa Olimpiki alianza vibaya 2023 baada ya kugundua kuwa akaunti yake, ambayo hajawahi kutoa au kuhamisha pesa tangu 2012, ilibaki na dola 12,000 pekee. Akaunti hiyo ilikuwa na $12.7 milioni kufikia Oktoba 31, 2022.
Kulingana na mawakili wa mwanariadha huyo, pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya kampuni ya kibinafsi ya uwekezaji ya Stocks and Securities Limited ya Jamaika (SSL) zilikusudiwa kutumika kama pensheni kwa mwanariadha huyo na familia yake.
Kulingana na ripoti nyingi, mpango wa udanganyifu wa SSL ulifikia zaidi ya dola milioni 30, na angalau akaunti 200 ziliathiriwa Januari mwaka jana, ikiwa ni pamoja na Bolt.
Akitumia mtandao wake wa kijamii siku ya Alhamisi, mwaka mmoja tangu kisa hicho, Bolt alichapisha ujumbe wa uthabiti kwa wafuasi wake milioni 13.8.
"Yow peeps, kwa hivyo imekuwa mwaka mmoja," alisema kwa lugha yake ya Jamaika. "Ninataka tu kuwajua kwamba bado mimi niko tu, bado ni pambano, pambano, bado mshikemshike, ninaendelea kuwa imara kila wakati. Yuh jua jinsi nchi vijana wanavyofanya (Nataka tu ujue bado niko hapa, nikipigana na kushikilia. Ninajaribu kuwa na nguvu. Kwa watu wote wanaoniunga mkono, endelezeni sapoti yenu. One love,” alisema.
Bolt hakurejelea moja kwa moja ulaghai wa SSL, lakini kulingana na muda wa wadhifa wake, ni wazi alikuwa anazungumzia hasara aliyoipata mwaka mmoja uliopita.