Kinda wa Barcelona, Lamine Yamal anazidi kuweka rekodi katika FC Barcelona kila kukicha kwa uchezaji wake wa ajabu akiwa na umri wa miaka 16 pekee.
Winga huyo mchanga wa Uhispania atafikisha umri wa miaka 17 mwezi huu wa Julai, na mchezaji huyo anatazamiwa kuendelea kuvunja rekodi zaidi huku akiendelea kuwa mchezaji bora.
Wakati Yamal akiwavutia mashabiki wa Barcelona kwa kuwa mchezaji muhimu wa timu katika umri mdogo, baadhi ya mashabiki wa Real Madrid wanaamini kwamba yeye ni mkubwa zaidi kuliko anachodai kuwa.
Lilianza wakati baadhi ya mashabiki wa timu pinzani walipotimba kwenye mtandao wa X wakidai kuwa na ushahidi kwamba Yamal ana miaka Zaidi ya 20 kama si kukaribia hapo, na wala si miaka 16 anavyodai.
Chapisho la X lilipendekeza kuwa Lamine Yamal alikuwa na umri wa miaka kumi mnamo 2015 kutokana na gazeti ambalo lilizungumza juu ya kijana huyo.
Yamal alikuwa amevalia jezi ya 2015/16 kwenye gazeti, ambayo iliakisi sifa za mchezaji huyo mchanga. Katika gazeti hilo, ilionyesha picha ya kijana Yamal na kusoma, "Tunafahamu kwamba tunazungumza juu ya mtoto ambaye ana umri wa miaka 10.”
Wengi walipinga madai hayo kwa kuwa gazeti lilichapishwa 2017, sio 2015. Ikiwa gazeti ilichapishwa mnamo 2015, itamaanisha kuwa mchezaji huyo kwa sasa ana miaka 18 sio 16.
Dai lingine linalopendekeza kwamba Yamal anadanganya kuhusu umri wake ni video ya YouTube inayoonyesha ujuzi wake na Youtuber uwanjani.
Video iliyopigwa tarehe 15 Machi 2021, ina jina linaloitwa "Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 16 ana yote kuwa mustakabali wa Barca!".
Hili limekanushwa kwenye video yenyewe wakati Youtuber na Lamine Yamal waliposema kuwa mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 13 wakati wa upigaji picha.
Hii kwa mara nyingine inathibitisha kwamba tetesi hizi za Yamal kuwa na umri wa zaidi ya miaka 16 ni uongo, na harakati ndogo kutoka kwa kikundi kidogo cha mashabiki wa Real Madrid ilitumia ushahidi wa uongo.
Baada ya mchezo wa Napoli kwenye Ligi ya Mabingwa, Lamine Yamal na FC Barcelona watacheza dhidi ya Atletico Madrid Jumapili kwenye La Liga.
Baada ya mapumziko ya kimataifa, Barcelona itacheza na Las Palmas nyumbani. El Clasico itachezwa mwezi ujao Santiago Bernabeu.