logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi wafanya winga wa Brazil Vinicius Jr ahisi 'hataki kucheza'

Vinicius Jr anasema anahisi "kana hatakii kucheza " kandanda kwa sababu ya unyanyasaji wa mara kwa mara wa kibaguzi aliofanyiwa.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo26 March 2024 - 04:12

Muhtasari


  • •Vinicius Jr anasema anahisi "kana hatakii kucheza " kandanda kwa sababu ya unyanyasaji wa mara kwa mara wa kibaguzi aliofanyiwa.
  • •Vinicius alisema: "Haikuniingia akilini [kuondoka Uhispania] kwa sababu nikiondoka Uhispania nitawapa wabaguzi kile wanachotaka.

Winga wa Brazil Vinicius Jr anasema anahisi "kana kwamba hataki kucheza " kandanda kwa sababu ya unyanyasaji wa mara kwa mara wa kibaguzi aliofanyiwa.

Msimu uliopita kulikuwa na matukio 10 ya aina hiyo dhidi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yaliyoripotiwa kwa waendesha mashtaka na La Liga.

Wakati wa mkutano wa wanahabari wenye hisia siku ya Jumatatu, Vinicius aliongeza kuwa hatalazimishwa kuondoka Real Madrid na Uhispania na kuruhusu ubaguzi wa rangi kushinda.

Hata hivyo, alisema alikuwa anaona ni "vigumu kusonga mbele" kutokana na unyanyasaji huo.

Brazil itamenyana na Uhispania katika mechi ya kirafiki ya kimataifa katika uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid siku ya Jumanne kama sehemu ya kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi chini ya kauli mbiu 'Ngozi moja'.

Vinicius alisema: "Haikuniingia akilini [kuondoka Uhispania] kwa sababu nikiondoka Uhispania nitawapa wabaguzi kile wanachotaka.

“Nitabaki kwa sababu kwa njia hiyo wabaguzi wa rangi wanaweza kuendelea kuniona usoni zaidi na zaidi.

“Mimi ni mchezaji shupavu, nacheza Real Madrid na tunashinda mataji mengi na hilo haliwafurahishi watu wengi.

"Nataka tu kucheza kandanda lakini ni vigumu kusonga mbele; najihisi kutopenda kucheza."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved