Kiungo wa kati wa Manchester United, Mason Mount hatmaye amekata kiu yake ya muda mrefu ya kupata bao, ikiwa ni tangu Desemba 2022 alipofunga bao lake la mwisho akiwa mchezaji wa Chelsea.
Mount alisajiliwa na United kutoka Chelsea msimu wa joto mwaka jana na tangu hapo hajapata wakati mzuri wa kucheza, akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.
Baada ya kurejea kutoka majeruhi, Mount alifunga bao la muhimu na lake la kwanza kama mchezaji wa Man Utd katika sare yao ya 1-1 dhidi ya Brentford usiku wa Jumamosi.
The Red Devils walidhani walikuwa wamepokonya pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Gtech Community baada ya Mason Mount kufungua akaunti yake kwa klabu hiyo kunako dakika ya 6 kati ya 9 za nyongeza.
Lakini hawakuweza kushikilia ushindi huo, kwani Brentford walisawazisha dakika tatu baadaye baada ya Kristoffer Ajer kufunga bao lililopikwa na Ivan Toney.
Na haikuwa kitu kidogo kuliko kile ambacho The Bees walistahili kuwa na mikwaju 31 langoni ikilinganishwa na 11 kutoka kwa Mashetani Wekundu.
Vijana wa Thomas Frank waligonga mbao mara nne huko Magharibi mwa London, na watabaki wakishangaa jinsi hawakuibuka washindi.
Brentford pia ni timu ya kwanza msimu huu kujivunia angalau miguso 80 ndani ya kisanduku cha wapinzani, jarida la talkSPORT lilieleza.