logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kipa wa Burundi azungumzia kikosi cha Harambee Stars

Kipa wa Burundi,Nahimana anatarajia mechi ngumu baina ya Kenya na Burundi ila ushindi kwa Burundi mwishowe.

image
na Davis Ojiambo

Michezo06 June 2024 - 13:39

Muhtasari


  • •Golikipa wa Burundi Jonathan Nahimana ametaja mchezo wa kesho Ijumaa 7 kuwa ngumu ila Burundi watanyakua ushindi.
  • •Kipa huyo amewatahadharisha wenzake kuwa makini dhidi ya wachezaji wa Kenya kama vile Muguna.

Mlinda lango wa Burundi Jonathan Nahimana amekitaja kikosi cha Harambee Stars kuwa bora zaidi ikilinganishwa na kile cha Burundi.

Kwenye mahojiano na sports boom,Nahimana amekitaja kikosi cha Harambee Stars kuwa na wachezaji bora huku akisema  nia yao ni kulipiza kisasi dhidi ya Harambee Stars, ambao waliwashinda katika michuano ya CECAFA Challenge Cup 2017 iliyofanyika nchini Kenya mara ya mwisho walipomenyana.

Nahimana ambaye  anachezea timu ya Namungo inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania ameichezea Burundi kwa  mechi 34, anaamini kwamba nchi zote mbili zina kile kinachohitajika kurejea kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) na kukata tikiti ya kombe la Dunia.

"Kenya na Burundi zina nafasi ya kweli ya kufuzu kombe la dunia ,kila mtu anadhani Ivory Coast itachupa virahisi,lakini soka imebadilika na hakuna tena timu ya chini.Ubora wa Kenya na Burundi ni mzuri vya  kutosha na haupaswi kupuuzwa..." Nahimana alisema.

Kipa huyo mwenye uzoefu alikuwa langoni katika mechi ya mwaka wa  2017 na anatarajiwa kuweka nafasi yake katika pambano la kesho Ijumaa 7  dhidi ya Kenya litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu. Kabla ya pambano hilo, Nahimana, ambaye amekuwa mwanzilishi anayependekezwa kwa muda mrefu, anatarajia mechi ngumu na ushindi kwa Burundi mwishoni.

"Bado nina kumbukumbu za kushindwa kwa CECAFA na Kenya karibu miaka saba iliyopita. Tunakutana tena  katika mchezo muhimu sana,” Nahimana alisema

"Itakuwa ngumu kwani timu zote mbili zinatoka mkoa mmoja, na kila moja itakuwa ikijitahidi kupata ushindi.."

Aidha mlinda lango huyo amesema kuwa matayarisho kwa upande wao yamekuwa bora na wanasubiri kwa hamu na ghamu kutifuana na Kenya.

"Maandalizi yetu yanaendelea vizuri kwani wachezaji wa ndani na wachezaji wachache wa kimataifa tayari wako kambini," alisema

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved