logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Droo ya kufuzu Afcon 2025 kufanyika Julai 4 kule Afrika Kusini

Droo ya kufuzu Afcon 2025 itafanyika Julai 4,2024 jijini Johannesburg,Afrika Kusini.

image
na Davis Ojiambo

Michezo13 June 2024 - 12:23

Muhtasari


  • •Droo ya kufuzu  mashindano ya Afcon 2025 inatazamiwa kufanyika Julai 4, jijini Johannesburg Afrika Kusini.
  • •Jumla ya timu 24 zinatazamiwa kufuzu kwenye mashindano hayo yanayoratibiwa kufanyika nchini Morocco.

Droo ya kufuzu mashindano ya Afcon 2025 itafanyika Julai 4,jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Jumla ya timu 48 ikiwemo Chad,Eswatini,Liberia na Sudan Kusini zitapangwa katika makundi 12 ya timu nne  kila moja ili kushindania nafasi za kufuzu kwa mashindano ya Afcon 2025.

Mechi hizo za kufuzu zinatazamiwa kuanza Septemba,2024 ili kuamua timu 24 zitakazoshiriki kwenye mashindano ya 2025,nchini Morocco.Wenyeji Morocco tayari washajinyakulia nafasi kwa kuwa mashindano yatafanyika kwao.

 Makala ya mwisho ya mashindano haya yalifanyika mwaka 2023 nchini Ivory Coast,huku wenyeji hao wakinyakua taji hilo kwa mara ya tatu baada ya kuwafunga wenzao Nigeria kwenye fainali.

Hata hivyo,tarehe za fainali za Afcon 2025 bado hazijatangazwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Hapo awali CAF ilijitolea kuandaa michuano yake bora ya wanaume mwishoni mwa msimu wa vilabu vya Ulaya,katika kipindi cha Juni-Julai.Wakati huo mechi za  kombe la klabu la dunia 2025 zitakuwa zikichezwa.

Mapema mwezi huu katibu mkuu wa CAF,Veron Mosengo-Omba aliambia BBC Sport Africa kwamba kupanga ratiba ni "ndoto" na akakiri kwamba huenda fainali za 2025 zikachezwa mapema 2026.

"Tunahitaji kuhakikisha kuwa tarehe ambazo tutakuwa tunachagua zitakuwa kwa maslahi ya wachezaji," Veron alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved