logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Roberto Firmino na mkewe waanzisha kanisa la kiinjilisti nchini Brazil

Roberto Firmino pamoja na mkewe Larissa wameanzisha kanisa lao nchini Brazil.

image
na Davis Ojiambo

Michezo09 July 2024 - 12:11

Muhtasari


  • •Firmino na mkewe walihamasishwa na imani yao thabiti kuanzisha kanisa  ili kueneza neno la Mungu na kusaidia jamii kupitia mafundisho.
  • •Nyota huyo wa Brazil  alihamia kwenye ligi kuu ya Saudi baada ya kuondoka Liverpool,huku akiwa ameshinda mataji tajika kama vile kombe la klabu bingwa Ulaya.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Roberto Firmino pamoja na mkewe Larissa wameanzisha kanisa la kiinjilisti nchini Brazil.

Nyota huyo wa zamani wa Brazil aliwekewa upako katika kanisa lililoanzishwa katika mji aliozaliwa wa Maceio. Uwekaji wakfu ulifanyika Jumapili iliyopita, Juni 30,2024.

Katika chapisho la pamoja kwenye Instagram,mchezaji huyo wa  umri wa miaka 32 na mkewe Larissa walielezea hafla hiyo kama "ya kukumbukwa na isiyoweza kusahaulika".

Pia waliongeza:

“Kutokana na kukutana kwetu na Kristo, hamu inawaka mioyoni mwetu: ili watu wajue upendo huu ambao umetufikia. Sasa tuna shauku na wajibu mwingine: kuwa wachungaji wanaoupendeza moyo wa Mungu na wanaoshirikiana na Ufalme."

Mnamo 2020, mshambuliaji huyo alibatizwa kwenye bwawa la kuogelea kwenye nyumba ya mchezaji mwenzake wa zamani Alisson.

Hata hivyo,Firmino amekuwa  akishiriki ujumbe wa kidini kwenye ukurasa wake na vijisehemu vyake akihubiri.

Staa huyo alijiunga na  Al-Ahli ya Saudi Pro League mnamo 2023 na tangu wakati huo amecheza mechi 34 na kufunga mabao tisa.

Aidha ,ameshinda taji la  ligi ya mabingwa , 2021-22 na klabu ya Liverpool.Firmino alichezea wekundu wa Anfield  kwa miaka minane na kuunda safu ya ushambuliaji ya ajabu akiwa na Mohamed Salah na Sadio Mane.

Wakati akiwa katika klabu hiyo, mbrazil huyo pia alishinda ligi kuu, kombe la FA na kombe la EFL. Kwa taifa lake, aliichezea Brazil mechi 55 na ndiye mbrazil aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye ligi kuu akiwa amefunga mabao 82.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved