logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arsenal yatangaza kikosi kitakachosafiri kwa michuano ya maandalizi ya msimu mpya

Declan Rice, Aaron Ramsdale, Bukayo Saka, David Raya na William Saliba wataungana na wenzao watakaporejea kutoka Amerika.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo22 July 2024 - 05:29

Muhtasari


  • •Arsenal inawakosa wachezaji wake muhimu Bukayo Saka, Kai Havertz, Declan Rice, William Saliba, Gabriel Magalhães na Gabriel Martinelli wanaposafiri kuelekea Marekani.
  • •Declan Rice, Aaron Ramsdale, Bukayo Saka, David Raya na William Saliba wataungana na wenzao watakaporejea kutoka Amerika.

Klabu ya soka ya Uingereza, Arsenal inawakosa wachezaji wake muhimu Bukayo Saka, Kai Havertz, Declan Rice, William Saliba, Gabriel Magalhães na Gabriel Martinelli wanaposafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya michezo yao ya kabla ya msimu mpya.

Klabu hiyo yenye maskani yake jijini London wiki hii itaanza michezo yao ya maandalizi kabla ya msimu wa EPL wa 2024/25 itakayoanza mwezi ujao.

Katika taarifa yake Jumapili, klabu hiyo ilitangaza kikosi cha wachezaji ishirini na sita, wakiwemo vijana wengi ambacho kitakuwa Marekani kwa ajili ya michezo ya maandalizi.

Wachezaji waliosafiri ni pamoja na;

Makipa: Karl Hein, Tommy Setford, Lucas Nygaard, Alexei Rojas

Mabeki: Ben White, Oleksandr Zinchenko, Jurrien Timber, Josh Nichols, Jakub Kiwior, Ayden Heaven, Omar Rekik

Viungo wa kati: Thomas Partey, Jorginho, Michal Rosiak, Myles Lewis-Skelly, Martin Odegaard, Emile Smith Rowe, Fabio Vieira, Ethan Nwaneri, Salah–Eddine Oulad M’Hand, Jimi Gower

Washambuliaji: Leandro Trossard, Reiss Nelson, Charles Sagoe Jr, Gabriel Jesus, Eddie Nketiah

Klabu hiyo ilitangaza kuwa kutokana na maendeleo yao katika michuano ya Copa America na Euro, Gabriel Magalhaes, Gabriel Martinelli na Kai Havertz watajiunga na kikosi hicho kuanzia Julai 25.

Wachezaji walioshiriki katika hatua za mwisho za Euro 2024 - Declan Rice, Aaron Ramsdale, Bukayo Saka, David Raya na William Saliba - wataungana na wenzao watakaporejea kutoka Amerika.

Mabeki Kieran Tierney na Takehiro Tomiyasu watasalia jijini London kupokea matibabu kutoka kwa wahudumu wetu wa afya huku wakipambana na majeraha ya msuli wa paja na goti mtawalia.

Katika ziara yao ya Marekani, wanabunduki wanatarajiwa kucheza dhidi ya Manchester United Julai 27, Liverpool Julai 31, Bayer Leverkusen Agosti 7 na Olympique Lyonnais Agosti 11.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved