Baada ya Meneja wa Girona FC, Miguel Ángel Sánchez Muñoz (Michel), kutazama mafunzo ya Savinho kwa mara ya kwanza wakati wa maandalizi ya msimu uliopita, mara moja alimpigia simu mkurugenzi wa michezo wa Girona, Quique Carcel.
"Tutamaliza katika nafasi ya nane bora," alimwambia Carcel.
Girona ilipigania taji la La Liga hadi mwisho. Walimaliza katika nafasi ya tatu - nyuma ya Real Madrid na Barcelona pekee.
Kufuzu na kuingia Ligi ya Mabingwa. Yalikuwa ni mafanikio makubwa zaidi katika historia ya miaka 93 ya klabu hiyo.
Katika muda wa mwaka mmoja, Savinho alitoka kuwa mchezaji wa akiba wa PSV Eindhoven ya Netherlands, hadi kuwa nyota anaechipukia nchini Uhispania.
Labda ndiye mchezaji mwenye kipaji cha kushangaza zaidi kwenye La Liga, ukizingatia kwamba [Jude] Bellingham alikuwa tayari anajulikana na kila mtu.
Haishangazi kwamba Manchester City wamefanya usajili wao wa kwanza wa Savinho msimu wa joto, na kumchukua kutoka timu ya Troyes, ambayo ilikuwa imempeleka kwa mkopo Girona.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amemaliza msimu uliopita akiwa na mabao 11 na pasi za mwisho 10 akiwa na Girona.
"Nilizaliwa na kipawa cha kucheza soka," husema mara kwa mara.
Kocha wa City Pep Guardiola sasa ana matumaini ya kufanya vizuri zaidi.
‘Mtoto huyu atakuwa mwanasoka'Amekulia katika nyumba ya babu na bibi, katika eneo la mashambani la Sao Mateus, kusini-mashariki mwa Brazili, alijifunza mapema kupanda farasi, kukama ng'ombe na kupanda mboga kama vile bamia na nyanya. Huko ndipo mahali pa likizo yake hadi sasa.
"Ukimuuliza kama anataka kutumia likizo yake Cancun, Mexico au kwa babu na bibi yake, bila shaka atachagua kwa babu na bibi," mama yake, Dona Nilma anasema.
Savinho alifurahia maisha ya kila siku shambani, hata hivyo, alikuwa ni mwanasoka mzuri.
Haikuchukua muda mrefu kwa Nilma kujua hilo - alikuwa na miaka mitano tu aliposikia utabiri kutoka kwa mmoja wa makocha wake wa awali.
"Mtoto huyu atakuwa mwanasoka," alitabiri.
Savinho alianza kucheza ufukweni, na baada ya kuhamia katika viwanja vya kawaida, akaanza kuingia kwenye rada ya timu kubwa.
Hatimaye, mchezaji huyo wa mguu wa kushoto alisajiliwa na Atletico Mineiro, ya Brazil baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye mechi dhidi ya timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Alikuwa na umri wa miaka 11.
Akiwa na umri wa miaka 16, akawa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuichezea Atletico kwenye ligi ya Brazil, akiwa na umri wa miaka 18, akawa mchezaji mdogo zaidi kuwafungia bao katika mchezo wa Kombe la Libertadores.
Kupanda kwake kuliishawishi Man City kumsogelea haraka na ikashinda ushindani kutoka kwa Arsenal na kupata saini yake 2022.
Mchezaji wa mabao 10
Savinho awali alisajiliwa katika klabu ya daraja la tatu ya Troyes, huko Ufaransa lakini hakuwahi kuitumikia timu hiyo ana akapelekwa kwa mkopo katika timu ya PSV ya Netherlands.
Jeraha la mapema, lilikwamisha maendeleo yake na kufanya iwe vigumu kung'ara katika ligi kuu ya soka ya Netherlands, iitwayo Eredivisie.
Timu ya Girona ilimwona kupita Kombe la Dunia la chini ya miaka 20, 2023 na ikaamua kuwa anastahili kununuliwa, ingawa haikuwa rahisi kumshawishi kocha Michel mwanzoni kwani aliomba winga mzoefu.
"Savinho hakuwa na uzoefu sana; alikuwa nje ya PSV, alicheza kama mchezaji wa akiba, si kama mchezaji wa kwanza, hivyo ilikuwa vigumu kupata mnunuzi," anasema Carcel.
Hivyo ilipigia afanye juhudi kubwa alipowasili Catalonia, Spain.
"Una uwezo wa kumaliza msimu huu ukiwa na mabao 10 na pasi za mabao 20, fanya hivyo," Michel alimwambia wakati wa mapumziko katika mechi ambayo tayari alikuwa amefunga na kutoa pasi ya mwisho moja.
Hakika haitakuwa rahisi kwa Savinho chini ya Guardiola. Lakini hajali. Anaziishi ndoto zake.