Mchambuzi mkongwe wa michezo ameondolewa katika jukumu lake la Olimpiki baada ya kutoa matamshi ya ngono kuhusu waogeleaji wa kike wa Australia kufuatia ushindi wao wa medali ya dhahabu.
Wakati timu ya mbio za mita 4x100 za kupokezana vijiti ilipokuwa ikitoka kwenye bwawa huko Paris,mchambuzi wa michezo ya Olimpiki afutwa kufuatia matamshi ya ngonoalisema "wanamalizia", na kuongeza "unajua jinsi wanawake walivyo... kuzurura, wakijipodoa".
Video hiyo ilisambaa haraka na mtangazaji wa Eurosport baadaye alisema alikuwa ameondolewa kwenye safu ya kuchambua.
Ballard bado hajatoa maoni yake hadharani kuhusu matamshi yake.
Mollie O'Callaghan, Emma McKeon, Meg Harris na Shayna Jack walikuwa wametoka kuzishinda Marekani na Uchina, na kushinda Olimpiki ya nne mfululizo ambapo Australia imetwaa medali ya dhahabu katika mashindano hayo.
Walikuwa wakipungia mkono umati na kusherehekea mafanikio wakati Bw Ballard alipotoa maoni yake.
Mchambuzi mwenzake na bingwa wa kuogelea wa Uingereza Lizzie Simmonds mara moja alitaja matamshi yake "ya kuchukiza", na kusababisha kicheko kutoka kwa Ballard.
Siku ya Jumapili, Eurosport ilidai kuwa Ballard - ambaye hapo awali alikuwa ripota wa muda mrefu wa BBC na mtangazaji - hatarejea mawimbi yao ya anga.
"Wakati wa sehemu ya matangazo ya Eurosport jana usiku, mtangazaji Bob Ballard alitoa maoni yasiyofaa," mtangazaji alisema katika taarifa.
"Kwa maana hiyo, ameondolewa kwenye orodha yetu ya kutangaza mara moja."
Bw Ballard amekuwa gwiji wa utangazaji wa michezo duniani tangu miaka ya 1980, akiripoti kuhusu michezo mingi ya Olimpiki na mashindano ya dunia.
Ametoa maoni mengi ya michezo ikiwa ni pamoja na hoki ya barafu na tenisi ya kiti cha magurudumu, lakini anajulikana zaidi kwa uchezaji wake wa kuogelea na kupiga mbizi.