Jepchirchir havunja rekodi ya ulimwengu huku akirudisha taji ya mbio hizo

Muhtasari
  • Jepchirchir havunja rekedi ya ulimwengi katika mbio za wanawake za half marathon
  • Mwanariadha huyo alimaliza kwa saa moja dakika tano na sekunde kumi na sita.

Mwanariadha Jere Jepchirchir ameshinfa katika mbio za half marathon kwa saa 1 dakika 5 na sekunde 16.

Ijumaa Jepchirchir alionya ulimwengu kuwa rekodi aliorekodi mnamo Septemba nchini Valencia kwa saa moja dakika 5 na sekunde thelathini na tano iko hatarini .

Huku mwanariadha akithibitisha maneno yake yalitimia baada ya kuvunja rekodi hiyo, alishinda taji hilo mnamo mwaka wa 2016.

Mjerumani Melat Yisak Kejeta alijishindia katika nafasi ya pili katika mbio hizo za wanawake kwa saa moja dakika tano na sekunde kuni na nane, huku mwanariadha Yalemzerf Yehualaw kutoka Ethiopia akishinda katika nafasi ya tatu kwa saa moja dakika tano sekunde kumi na tisa.

Aliyekuwa bingwa wa mbio hizo Joyciline Jepkosgei alimaliza nafasi ya sita kwa saa moja dakika tano na sekunde hamsini na nane