Muhtasari
- ‘ Ingawaje kulikuwa na upepo mkali nilimudu kukimbia vizuri’ amesema
- Muda bora Zaidi ulikuwa 14:44 uliosajiliwa na raia wa New Zealand Sifan Hassan mwaka wa 2019.
Mkenya Beatrice Chepkoech amesajili rekodi mpya ya dunia siku ya jumapili kwa kushinda mbio za kilomita tao huko Monaco .
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29 aliongeza sekunde moja kwa kusajili muda wa dakika 14 na sekunde 43 na kujizidishia rekodi kando na ile ya mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji .
‘ Ingawaje kulikuwa na upepo mkali nilimudu kukimbia vizuri’ amesema
Muda bora Zaidi ulikuwa 14:44 uliosajiliwa na raia wa New Zealand Sifan Hassan mwaka wa 2019.
Mganda Joshua Cheptegei ndiye aliyeshinda mbio hizo kwa upande wa wanaume kwa muda wa 13:13, nje ya rekodi yake ya 12.51 aliokuwa ameandikisha Monaco miezi 12 iliyopita .