Hongera!Faith Kipyegon aibuka mshindi katika fainali ya mbio za mita 1,500

Muhtasari
  • Faith Kipyegon aibuka mshindi katika fainali ya mbio za mita 1,500
Faith Kipyegon
Image: Hisani

Faith Kipyegon amepatia nchi ya Kenya dhahabu ya pili ya Olimpiki ya Tokyo kutokana na uushindi wake  katika fainali za wanawake za mita 1500.

 Sifan Hassan wa Uholanzi, alimaliza wa tatu baada ya shida kidogo katika hatua zake katika mita 200 za mwisho.

Kenya sasa ina dhahabu 2 katika mashindano ya olimpiki.

Kinara wa ODM Raial Odinga alichukua fursa hiyo na kumpongeza KIpyegon kwa ushindi wake.

Pia alimshauri mshindi huyo azidi kuhamasisha vijana.

Huu hapa ujumbe wake;

"Wow. Hiyo ni mbio nzuri.Hongera Faith Kipyegon kwa, kushinda medali ya dhahabu ya mita 1,500 na ​​kuweka Rekodi mpya ya Olimpiki.

Taifa zima linajivunia wewe kufanikiwa kutetea jina lako. Endelea kukimbia na endelea kuhamasisha vijana Hongera!," Aliandika Raila.