'Ndoto ya Olimpiki ni ndoto maalum,'Kipchoge azungumza baada ya kushinda dhahabu katika mbio za wanaume Tokyo

Muhtasari
  • Kipchoge azungumza baada ya kushinda dhahabu katika mbio za wanaume Tokyo
  • Eliud Kipchoge anyakua dhahabu katika mbio za wanaume Tokyo
Mwanariadha Eliud Kipchoge
Image: Twitter Kipchoge

Mmiliki wa rekodi ya mbio za marathon duniani Eliud Kipchoge aliweka historia baada ya kushinda dhahabu yake ya pili mfululizo katika mbio za wanaume katika Olimpiki za Tokyo 2020 Jumapili, Agosti 8.

Kipchoge alishinda kwa saa 2, dakika 8, na sekunde 38,Abdi Negeeye wa Uholanzi alichukua fedha wakati Bashir Abi wa Ubelgiji alipata shaba.

Mwenzake wa Kenya Lawrence Cherono aliibuka wa nne kwenye mbio na msimu bora wa masaa 2 dakika 10 na sekunde 2.

Mwanariadha ana rekodi rasmi ya mbio za ulimwengu za masaa 2 dakika 1 na sekunde 39 na rekodi ya saa 1 dakika 59 na sekunde 40 wakati wa INEOS 1:59 huko Vienna.

Ushindi wa Kipchoge katika hafla hiyo ilifunga dhahabu nyingine kwa nchi ya kenya.

 Kenya ilifanikiwa kupata dhahabu nne, medali nne za fedha, na medali mbili za shaba ktika hafla hiyo.

Licha ya kuanza polepole, Kenya ilifanikiwa kupata ushindi katika hafla hiyo ya kifahari.

Baada ya ushindi wake, kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliwahimiza wanariadha wengine kwa ujumbe huu.

"Ndoto ya Olimpiki ni ndoto maalum. Kwa kila mwanariadha hapa imechukua maandalizi ya maisha yote kufikia hatua hii

Leo naishi ndoto yangu ya Olimpiki. Daima nasema kwamba mchezo ni kama maisha, ambayo unaweza kushinda na kupoteza. Lakini leo ilikuwa siku ambapo nilishinda

Ninaweza kusema nilifanikiwa kutetea taji langu la Olimpiki. Nataka kushiriki shukrani kwa watu wa Japani na shirika la Olimpiki kwa kazi nzuri ya kufanya Olimpiki hizi zifanyike.

Dunia inayoendesha ni ulimwengu wenye furaha.#NoHumanIsLimited,"Aliandika Kipchoge.

Kutoka kwetu wanajambo Hongera Kipchoge kwa ushindi wako.