Mwanariadha Haile Gebrsellasie kujiunga na vita Ethiopia

Muhtasari

•Baadhi ya watu maarufu nchini Ethiopia wametoa tangazo kama hilo huku vita vikiendelea huku waasi wakitangaza kufanikiwa kuteka baadhi ya maeneo na sasa wanakaribia mjii mkuu wa Addis Ababa.

Mwanariadha wa zamani nchini Ethiopia Gebrsellasie
Mwanariadha wa zamani nchini Ethiopia Gebrsellasie
Image: AFP

Bingwa wa mbio za Olimpiki na mwanariadha wa zamani nchini Ethiopia Haile Gebrselassie ametangaza mipango ya kujiunga na jeshi la taifa lake siku moja tu baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutangaza kwamba anajiunga katika vita dhidi ya waasi kutoka jimbo la kaskazini la Tigray.

Pia miongoni mwa watakaojiunga katika vita hivyo ni mwanaraidha wa mbio ndefu Feyisa Lelisa ambaye alikuwa maarufu kwa pingamizi yake katika michezo ya olimpiki ya Rio alipoinua mikono juu ya kichwa chake – ishara iliotumika wakati huo na raia wa Ethiopia kupinga hatua ya serikali dhidi ya raia wa kabila la Oromo.

Baadhi ya watu maarufu nchini Ethiopia wametoa tangazo kama hilo huku vita vikiendelea huku waasi wakitangaza kufanikiwa kuteka baadhi ya maeneo na sasa wanakaribia mjii mkuu wa Addis Ababa.

Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na picha ya waziri mkuu Abiy Ahmed aliyeonekana akielekea katika vita hivyo akiwa amevalia magwanda ya kijeshi katika gari lililozungukwa na vikosi maalum.

Hatahivyo sio wazi kwamba Abiy amejiunga katika vita hivyo kwasababu BBC haikuweza kuthibitisha picha hizo.

Mazungumzo ya upatanishi yanayoongozwa na mjumbe wa Muungano wa AU , Olesegun Obasanjo bado hayajafua dafu.

Kufuatia ziara yake nchini Ethiopia wiki hii , mjumbe maalum kutoka Marekani katika eneo la upembe wa Afrika Jeffrey Feltman alisema kwamba wote waziri mkuu Abiy Ahmed na chama cha wapiganaji wa TPLF waliamini kwamba walikuwa