Ulijitahidi-Mkewe Omanyala ampongeza baada ya ushindi wa Mauritius

Muhtasari
  • Kulingana na mama wa mtoto mmoja, mpenzi wake alikuwa amejitahidi sana kustahili medali ya dhahabu
Ferdinand Omanyala
Ferdinand Omanyala
Image: HISANI

Lavender Omanyala, mke wa nyota anayechipukia kwa kasi Mkenya Ferdinand Omanyala hii leo ameelezea furaha yake baada ya ushindi wa mumewe katika Riadha za Kiafrika zilizoandaliwa Reduit, Mauritius.

Omanyala alifanikiwa kuondoka na medali ya dhahabu baada ya kuwabwaga wapinzani wake wote katika mbio za mita 100.

Omanyala inasemekana alitumia sekunde 9.927 kuwashinda wapinzani wengine wote akiwemo Ankani Simbine wa Afrika Kusini aliyeibuka wa pili.

Akiwa amefurahishwa na matokeo hayo, Lavender alitumia ukurasa wake wa Instagram huku akimmwagia sifa mchumba wake Ferdinand Omanyala.

Kulingana na mama wa mtoto mmoja, mpenzi wake alikuwa amejitahidi sana kustahili medali ya dhahabu.

"Ulijitahidi sana kuleta medali nyumbani...najivunia wewe. Utukufu, utukufu kwa Mwenyezi. Tazama mshindi wa medali ya dhahabu ya Ubingwa wa Wakubwa wa Afrika 2022,"Aliandika.

Sawa, uungwaji mkono wa Lavender kuelekea taaluma ya mumewe mara nyingi umekuwa mwingi sana.

Katika mahojiano ya awali katika kipindi cha Jeff Koinange Live, Ferdinand Omanyala hata alifichua kuwa mke aliwahi kumfadhili kifedha wakati fulani ambapo mambo bado hayakuwa sawa kwake.

Kutoka kwetu wanajambo Hongera Ferdinand Omanyala kwa mafanikio yako mapya.