Faith Kipyegon aishindia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu huko Oregon

Hii pia ilikuwa ni medali ya nne ya dhahabu kwa Kipyegon katika 1,500, na fedha katika 2015 na 2019

Muhtasari

• Kipyegon alitumia 3:52.96 kuhifadhi taji aliloshinda mjini Doha mwaka wa 2019 huku Muethiopia Gudaf Tsegay akitwaa medali kwa saa 3:54.52. Laura Muir wa Uingereza alijishindia shaba kwa saa 3:55.26.

Mwanariadha Faith kipyegon akisherehekea katika mashindano ya awali
Mwanariadha Faith kipyegon akisherehekea katika mashindano ya awali
Image: The Star (Maktaba)

Bingwa mara mbili wa Olimpiki wa mbio za mita 1,500 Faith Kipyegon aliipatia Kenya medali ya kwanza ya dhahabu katika mbio za mita 1,500 kwa wanawake katika Riadha za Dunia zinazoendelea huko Oregon, Marekani.

Kipyegon alitumia muda wa 3:52.96 kuhifadhi medali hiyo aliyoshinda mjini Doha mwaka wa 2019 huku Muethiopia Gudaf Tsegay akitwaa medali kwa saa 3:54.52. Laura Muir wa Uingereza alijishindia shaba kwa saa 3:55.26.

Rekodi hii ya Kipyegon ni ya 10 kwa kasi zaidi kuwahi na ni mara ya 2 kwa kasi zaidi nchini Marekani, baada ya muda wake wa 3:52.59 kwenye mashindano ya Prefontaine ya 2022.

Kipyegon alishinda medali yake ya 2 ya dhahabu, akitoshana nguvu na wanariadha wengine 3 - Hassiba Boulmerka (Algeria), Tatyana Tomashova (Urusi), na Maryam Jamal (Bahrain), ambao hapo awali walichapisha mafanikio sawa kwa umbali.

Hii pia ilikuwa ni medali ya nne ya dhahabu kwa Kipyegon katika 1,500, na fedha katika 2015 na 2019, na anakuwa mkimbiaji wa kwanza kushinda medali nne katika mashindano hayo. Bingwa wa Afrika Winnie Chebet alimaliza wa mwisho kwa saa 4:15.13.

Alishinda mbio za vijana katika Mashindano ya Dunia ya 2011 na 2013, kabla ya kutawazwa bingwa wa Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2014, na mshindi wa Ligi ya Diamond 2017 na 2021.