Matayarisho ya Wachezaji kuhusu mashindano kule Birmingham.

Uongozi wa timu umehakikisha kwamba mahitaji zote kuhusu Michezo yapo

Muhtasari

Julai 17 timu ya kwanza ikiongozwa na mkuu wa michezo, John Ogolla na Afisa Mkuu Mtendaji, Humphrey Kayange waliondoka ili kuhakikisha mipango ya kutosha inafanywa ili kuipokea timu hiyo itakapowasili.

• Baadhi ya mambo kwenye orodha ni pamoja na; Visa, tikiti,  PRC na chanjo ya Covid-19,miongoni mwa zingine.

Wacheza wa Kenya wakiwa kwenye harakati ya maandalizi
Wacheza wa Kenya wakiwa kwenye harakati ya maandalizi
Image: STAR

Kundi la kwanza la Timu-Kenya linalojumuisha vitengo 11 linatazamiwa kusafiri Ijumaa kwa Michezo ya Jumuiya ya 'commonwealth' inayotarajiwa kuanza Julai 28 hadi Agosti 8 huko Birmingham.

Vitengo hizo tofauti ni pamoja na-riadha, ndondi, squash, hoki, badminton, baiskeli, kuogelea, tenisi ya meza, miongoni mwa mengine.

Games’ de Mission, John Ogolla, na afisa mkuu mtendaji, Humphrey Kayange waliondoka Jumapili kuhakikisha kila kitu kiko sawa kabla ya kufika  kwa timu hiyo.

Hii ikiwa ni mara ya 17  Kenya  kushiriki nchini humo katika Michezo ya Vilabu ambayo uandaliwa baada ya miaka minne, wanariadha wako tayari kwa siku 11 za mchezo zitakaonyeshwa moja kwa moja kwenye runinga ya KBC.

Uongozi wa timu umehakikisha kuwa maelezo yote kuhusu Michezo yapo, ikijumuisha  na ile ya kufuata  kanuni za Covid-19.

Majaribio ya PCR yalianza Jumatano katika Kambi ya Makazi katika Uwanja wa Moi Kasarani kwa timu zinazosafiri Ijumaa, kulingana na katibu mkuu wa Nock Francis Mutuku.

"Tuko tayari kwa Birmingham na wanariadha wote wana hati za kusafiria," Mutuku alisema.

Aliongeza: “Orodha ya ukaguzi imetolewa kwa wasimamizi wote wa timu kuhakikisha wana kila kitu ambacho timu inahitaji siku chache kabla ya kuondoka. Tuna furaha kuripoti kwamba kila kitu kiko sawa. Nike 'Kit' rasmi itatolewa leo''

Wanariadha ambao kwa sasa wako Oregon kwa Mashindano ya Dunia wataungana moja kwa moja na Birmingham kati kati ya wiki.