Natamani kukimbia na Obama - Eliud Kipchoge

Ningemwalika Kenya kushiriki mbio nami - Kipchoge.

Muhtasari

• Kipchoge alisema anaamini katika kukimbia na watu kwenye maundi kwani mbio ndio mashindano pekee ambayo huleta watu pamoja.

Kipchoge asema anatamani kushiriki mbio na Obama
Kipchoge asema anatamani kushiriki mbio na Obama
Image: Facebook

Mwanariadha wa masafa marefu Eliud Kipchoge ameweka wazi kwamba angependa sana siku moja kabla hajastaafu kutoka riadha ashiriki katika mbio hizo na aliyekuwa rais wa 44 wa Marekani Barrack Obama.

Jarida la Marca liliripoti kwamba Kipchoge aliulizwa hilo uzi akijiandaa katika mbio za Berline Huko Ujerumani ambapo alikuwa analenga kuvunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka katika mbio za awali.

Kipchoge aliulizwa ni mtu gani aliye hai au aliyekufa angependa kushiriki naye mbio za asubuhi.

Mwanariadah huyo, ambaye aliweka rekodi ya dunia ya saa 2:01:39 katika makala ya 2018 ya Berlin Marathon, alisema angemchagua Obama.

Alisema kwamba sababu zake za kumchagua rais huyo mstafu wa Marekani ni kutokana na jinsi anavyojiweka kiustaarabu na pia alifichua angependa sana kushiriki mbio hizo naye nchini Kenya.

"Nadhani ningemchagua Barack Obama. Ningemwalika Kenya kushiriki mbio nami. Sababu ni kwamba, Barack Obama ana tabia ya msukumo, tabia ya umoja, na inapita zaidi ya asili yote ya mwanadamu," Kipchoge alinukuliwa na jarida la Marca.

Itakumbukwa kwamba babake Barrack Obama ana asili yake nchini Kenya.

Mwanasiasa Kipchoge atakumbukwa pia kwa kuvunja rekodi ya mashindano ya Illeneos jijini Viena Austria mwaka 2019 alipotimuka saa moja na dakika hamsini na tisa na kuweka rekodi ambayo ilikuja kufahamika na wengi kuwa hakuna mwanadamu asiyeweza kufanya kitu cha kihistoria.

Alisema anaamini katika uwezo wa kukimbia kuwaunganisha watu.

"Kukimbia kunakuza uhuru wa kujumuika. Watu wanapokimbia pamoja, wanakuwa wamoja - na kunapokuwa na umoja, kuna amani. Tukimbie pamoja... tukimbie pamoja. Shughuli pekee, ambayo inaweza kutufanya tushikamane, ni kukimbia," Kipchoge alisema.