SIKU IMEWADIA

Ruth Chepng'etich kutetea taji lake la marathoni

Seifu Tura wa Ethiopia atakuwa akikodolea macho taji la wanaume kwa mara ya pili.

Muhtasari

•Chepng'etich anapigiwa upatu kushinda taji hilo ikizingatiwa kuwa tayari ameshinda marathoni sita kati ya nane alizomaliza hadi sasa. 

•Benson Kipruto, Bernard Koech, Elisha Rotich na Eric Kiptanui watasaka taji katika mbio za wanaume.

 

Ruth Chepng'etich
Ruth Chepng'etich
Image: HISANI

Mkenya, Ruth Chepng'etich, anatarajiwa kutetea taji lake la Chicago Marathon Jumapili jioni.

Wakenya wengine katika mbio hizo ni pamoja na bingwa wa Seoul Marathon Celestine Chepchirchir na bingwa wa Milan Vivian Kiplangat.

Watatu hao watakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Waethiopia Ruti Aga, Haven Hailu na Weganesh Mekasha.

Chepng'etich anapigiwa upatu kushinda taji hilo ikizingatiwa kuwa tayari ameshinda marathoni sita kati ya nane alizomaliza hadi sasa.

Ushindi wake wa hivi majuzi zaidi ulikuja Nagoya mapema mwaka huu alipovunja rekodi ya mwendo wa saa 2:17:18.

Wakati huo huo, katika mbio za wanaume, Wakenya Benson Kipruto, Bernard Koech, mshindi wa Paris Elisha Rotich na Eric Kiptanui watakuwa wakisaka kumenyana na Ethiopia.

Bingwa mtetezi Seifu Tura atakuwa akilikodolea macho taji hilo kwa mara nyingine.

Wanawake

Ruth Chepngetich (KEN) 2:17:08, Ruti Aga (ETH) 2:18:34, Celestine Chepchirchir (KEN) 2:20:10, Vivian Kiplagat (KEN) 2:20:18, Haven Hailu Desse (ETH) 2:20:19, Waganesh Mekasha (ETH) 2:22:45, Emily Sisson (USA) 2:23:08, Delvine Meringor (ROU) 2:24:32, Laura Thweatt (USA) 2:25:38, Sara Vaughn (USA) 2:26:53, Susanna Sullivan (USA) 2:26:56, Diane Nukuri (USA) 2:27:50

Wanaume

Herpasa Negasa (ETH) 2:03:40, Bernard Koech (KEN) 2:04:09, Elisha Rotich (KEN) 2:04:21, Dawit Wolde (ETH) 2:04:27, Seifu Tura (ETH) 2:04:29, Stephen Kissa (UGA) 2:04:48, Abayneh Degu (ETH) 2:04:53, Benson Kipruto (KEN) 2:05:13, Shifera Tamru (ETH) 2:05:18, Eric Kiptanui (KEN) 2:05:47, Kyohei Hosoya (JPN) 2:06:35, Hamza Sahli (MAR) 2:07:15, Amanuel Mesel (ERI) 2:08:17, Hiroto Fujimagari (JPN) 2:08:20, Guojian Dong (CHN) 2:08:26, Kiyoshi Koga (JPN) 2:08:30, Riki Nakanishi (JPN) 2:08:51, Jemal Yimer (ETH) 2:08:58.