Hongera!Hellen Obiri ashinda mbio za Boston Marathon kwa wanawake

Muhtasari
  • Chebet alikuwa akitetea ushindi wake katika Marathon ya wanaume baada ya kushinda mwaka jana.
HELLEN OBIRI
Image: KWA HISANI

Mwanariadha wa Kenya Hellen Obiri ameshinda mbio za Boston Marathon.

Bingwa huyo wa mbio za mita 5,000 alikata mkanda huo kwa muda wa 2:21:38.

Obiri alicheza marathon kwa mara ya kwanza mwaka jana alipokimbia New York City Marathon ambapo alishika nafasi ya sita.

Ushindi wake unakuja baada ya Evans Chebet kutetea vyema taji lake la Boston Marathon mnamo Aprili 17, baada ya kutumia muda wa 2:05:54.

Chebet alikuwa akitetea ushindi wake katika Marathon ya wanaume baada ya kushinda mwaka jana.

Geoffrey Mutai anashikilia rekodi ya kozi ya Boston Marathon ya 2:03:02 kutoka 2011.

Zawadi ya fedha taslimu ya mshindi kwa wanaume na wanawake imepangwa kuwa dola 150,000 ambazo ni sawa na Sh20 milioni.

Kwa mshindi wa Medali ya Fedha, ambayo ni nafasi ya pili, washindi watachukua hadi dola 75,000 sawa na Sh10 milioni.