Ferdinand Omanyala apongeza serikali kwa kuwaunga mkono wanariadha

Omanyala ndiye mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika kwenye mbio za mita 100

Muhtasari

• Omanyala aliwapa motisha wanariadha wengi ambao hawajafanikiwa katika michezo yao akiwataka kutokata tamaa na kuendelea kufanya bidii kila.

Bingwa wa Afrika katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala
Image: TWITTER// FERDINAND OMANYALA

 Mshikilizi wa rekodi ya Afrika wa mbio za mita 100  Ferdinand Omanyala amepongeza serikali kwa ufhadhili inaotoa kwa wanariadha.

Mwanariadha huyo aliwapa matumaini wanariadha watarajiwa ambao wana ndoto ya kujiunga na mchezo huo kutia bidii.

"Tunapata furaha kutoka kwa serikali wakati tunapofanya vyema katika mashindano yetu licha ya kukumbwa na changamoto nyingi serikali yetu inafanya michezo yetu kuwa rahisi kwa kutupa fedha za kufanikisha  mbio zetu kwa wakati ufaao",alisema.

Mwanariadha huyu pia aliwapa motisha wanariadha wengi ambao hawajafanikiwa katika michezo yao akiwataka kutokata tamaa na kuendelea kufanya bidii kila wakati ndiposa siku moja wapate kufurahia jasho lao.

Omanyala aliwataka wazazi na walezi kuwaunga mkono watoto wao katika kila wanachofanya,  ili kuanza kukuza vipawa vyao mapema ndiposa wafanikiwe kwa maisha kupitia talanta zao mbalibali.

"Maisha sio rahisi watu wanatuona kwenye Runinga  na kudhani tumefika huko kwa bahati lakini hatufiki huko kwa bahati nzuri  ila tumejitahidi sana kufika huko, na tumekuwa na dhamira, uthabiti na uvumilivu kumfikisha mtu yeyote pale", alisema.