• Andrew Kiptoo Alamisi mwenye umri wa miaka kumi na 17 alishinda dhahabu katika mashindano ya dunia kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20, katika mbio za mita 5000 ,na kuwapiku wanariadha kutoka Uhabeshi na Uganda.
Andrew Kiptoo Alamisi mwenye umri wa miaka kumi na 17 alishinda dhahabu katika mashindano ya dunia kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20, katika mbio za mita 5000, na kuwapiku wanariadha kutoka Uhabeshi na Uganda.
Alamisi alishinda mbio izo za ufunguzi kwa kutumia mda wa 13:41:14 na kuwapiku wapinzani wake wa karibu kutoka Uhabeshi na Uganda waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia ambao ni Abdisa Fayisa na Keneth Kiprop.
Kwenye mbio hizo ambapo Alamasi alionekana kulemewa katika hadi ilipofikia katika lapu ya mwisho ambapo alitimuka na kunyakua ushindi .
Aidha,Alamisi alifungua orodha ya utwaaji medali katika mashindano hayo ambayo yalishika kasi siku ya jana kwa Taifa la Kenya,na kuandikisha mda wake bora katika mbio hizo.
Kenya sasa inalenga angalau kushinda zaidi ya medali kumi ili kupiku medali walizotwaa katika makala yaliyopita yaliokuwa yameandaliwa Cali,Colombia na ambapo Taifa la Kenya lilimaliza katika nafasi ya nne.
Michezo hiyo inatarajiwa kuendelea hadi tarehe 31 agosti huku Kenya wakiwa na matumaini ya kufanya vyema .