•Mwanariadha kutoka Taifa la Botswana Lesley Tebogo,alishinda katika mbio za mita mia 200, na kutwaa ushindi huo,huku akimpiku mwanariadha Kenneth Bednareck kutoka Amerika.
•Teboga,alishinda kwa mda wa 19.55, na sasa atakuwa anashiriki katika fainali za Wanda Diamond League,ambazo zitaandaliwa mjini Brussels,Ubelgiji kati ya tarehe 13 na 14 septemba 2024.
Mwanariadha kutoka taifa la Botswana sasa anazidi kufanya vyema katika mashindano ya mbio za mita 200.Hiii inajitokeza baada ya Tebogo kushinda katika mashindano ya Diamond League kwenye mbio za mita 200 kwa mda wa 19.55.
Tebogo ,aliwapiku wapinzani wa karibu wakiwemo Kenneth Bednareck,Knighton Erriyon na Fred Kerly wote kutoka America.
Tebogo,amekuwa akishamiri baada ya kushinda katika mbio hizo katika michezo ya olimpiki iliyoandaliwa Paris,na kumshinda Noah Lyles wa America ambaye amekuwa akitawala kwa kipindi kirefu katika mbio hizo.
Tebogo,amekuwa mwanariadha wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 200 Afrika na vile vile Botswana.Ikubukwe kwamba Tebogo ambaye alimpoteza mamake mzazi mapema mwaka huu,alichukua fursa hiyo kumshabikia mamake na dhahabu aliyoishinda Paris,michezo ya olimpiki.
Mbio hizo zilikuwa zake za mwisho katika michezo ya Diamond League ,kabla yake kusafiri kwenda katika fainali ambazo zitakuwa zimeandaliwa katika mji wa Brussels,Ubeligiji kati ya tarehe 13 na 14, septemba 2024 ikiwa ni fainali za Wanda Diamond League na ambapo anatarajiwa kutamba.