Bondia Conjestina Achieng ateketeza nyumba yake

Hakuna mali iliyookolewa kulingana na kaka yake William Ochieng.

Muhtasari

• Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Gem Charles Chacha alisema kuwa wanamtafuta bondia huyo ambaye alikuwa ametoroka

Bondia Conjestina Achieng
Bondia Conjestina Achieng
Image: MAKTABA

Bondia mashuhuri Conjestina Achieg Ijumaa asubuhi aliteketeza nyumba yake.

Hakuna mali iliyookolewa kulingana na kaka yake William Ochieng.

Ijumaa kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Gem Charles Chacha alisema kuwa wanamtafuta bondia huyo ambaye alikuwa ametoroka.

"Tutamkamata. Atakamatwa kwa kuchoma nyumba," alisema.

Kaka yake alisema waliamka saa kumi na moja asubuhi na kuona nyumba hiyo ikiwaka moto.

"Tuna changamoto nyingi kukaa naye nyumbani kulingana na hali yake ya sasa," alisema.

OCPD alisema kuwa kwa muda sasa, afya ya bondia huyo imekuwa ikizorota.

"Tumekuwa tukipata habari juu ya afya yake. Kwa bahati mbaya amekunywa pombe kupita kiasi na mara nyingi huwa mkali," alisema.

Odhiambo alisema kuwa hawajapata amani tangu bondia huyo aje nyumbani.

"Anampiga kila mtu. Tumetoa ripoti kadhaa kwa polisi na wasimamizi wa eneo hilo bila msaada wowote," alisema