Mwanabondia wa Tanzania afariki dunia baada ya kuanguka ulingoni wakati wa pambano

Bondia huyo alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa lakini afya yake ilidorora ghafla siku nne tu baadae akiwa bado hospitalini.

Muhtasari

• Bondia huyo alikuwa ndio mwanzo ameshiriki mapambano matatu tu ya ngumi kulipwa. Najum alikuwa ameshinda pambano moja tu na kupoteza mawili.

Bondia wa Tanzania afariki ulingoni.
Bondia wa Tanzania afariki ulingoni.
Image: Screengrab

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Tanzania Ibrahim Najum kutoka jiji la Mbeya ameripotiwa kufariki dunia baada ya kuanguka ulingoni Jumapili iliyopita mara baada ya kumalizika kwa pambano lake.

 Vyanzo vya habari kutoka nchini humo viliripoti kwamba Najum alifariki mapema Alhamisi katika hospitai ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokuwa akipokea matibabu tangu wikendi iliyopita alipoanguka ulingoni.

Najum aliripotiwa kuanguka ulingoni Jumapili iliyopita ulingoni mara bada ya kumalizika kwa pambano lake la awamu ya nne dhidi ya Bondia wa Dodoma Lawrence Segu.

Bondia huyo inaarifiwa alifanyiwa upasuaji mdogo eneo la kichwani na hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na umauti katika siku hiyo ya Ijumaa.

Bondia huyo alikuwa ndio mwanzo ameshiriki mapambano matatu tu ya ngumi kulipwa. Najum alikuwa ameshinda pambano moja tu na kupoteza mawili.