Mandonga Mtu Kazi na Wanyonyi kuzichapa tena mwezi Julai

Mandonga alimshinda Wanyonyi walipokutana kwa mara ya kwanza Januari 14, mwaka huu

Muhtasari

•Ijumaa walibadilishana maneno ya kukosoana kama ilivyo kwa wapinzani kabla ya mechi yao ya marudiano iliyokuwa ikitarajiwa kufanyika jijini Nairobi.

Image: BBC

Baada ya pambano la kufana la kwanza miezi minne iliyopita, sasa wanasema usubiri kwa ghamu pambano la marudiano la uzito wa juu la “Mandonga na Wanyonyi 2” ambalo linaahidi kutingisha Kituo cha Maonyesho cha Sarit Julai 22, mwaka huu, kulingana na gazeti la Daily Nation.

Mwanandondi wa Tanzania, Karim maarufu kama “Mtu Kazi” Mandonga, ambaye ni bingwa wa Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST), na Daniel Wanyonyi, bingwa wa zamani wa taji la Afica Boxing Union (ABU) Kenya, Ijumaa walibadilishana maneno ya kukosoana kama ilivyo kwa wapinzani kabla ya mechi yao ya marudiano iliyokuwa ikitarajiwa kufanyika jijini Nairobi.

Afisa mkuu mtendaji wa kusimamia mashindano wa Ultra Fight Series Maurice Odera alifichua Ijumaa kuwa Mandonga na Wanyonyi wametia saini mkataba wa kukutana tena kwenye mchuano wa "Marudio au Kulipiza kisasi"

Mandonga alimshinda Wanyonyi walipokutana kwa mara ya kwanza Januari 14, mwaka huu katika ukumbi wa KICC.