Drake ameweka bet ya Ksh 73m kwa mchezo wa ngumi Mnaijeria kumshinda Mmarekani

Iwapo Mnaijeria huyo Israel Adesanya atafaulu kumchachafya Mmarekani Sean Strickland, basi Drake ataondoka na kitita cha shilingi 134,458,000.00 ikiwa ni faida ya zaidi ya milioni 63 za Kenya kwa bet moja.

Muhtasari

• Mcheza kamari huyo wa kudumu alichapisha karatasi ya dau kwenye ukurasa wake wa Instagram bila nukuu.

• Mechi ya Adesanya dhidi ya Sean Strickland ya UFC 293 itakuwa tarehe 10 Agosti saa 2 asubuhi GMT.

Drake
Drake
Image: Insta

Nguli wa muziki wa rap kutoka Kanada, Drake kwa mara nyingine ameonesha Imani aliyo nayo kwa mchezaji wa ndondi kutoka New Zealand mwenye asili ya Nigeria, Israel Adesanya.

Drake ameweka mkeka wa dau la dola nusu milioni – kiasi sawa na shilingi za Kenya milioni 73 – kwa pambano la UFC 293 ambalo litawakutanisha Adesanya na bondia kutoka Marekani Strickland Sean.

Mcheza kamari huyo wa kudumu alichapisha karatasi ya dau kwenye ukurasa wake wa Instagram bila nukuu.

Mechi ya Adesanya dhidi ya Sean Strickland ya UFC 293 itakuwa tarehe 10 Agosti saa 2 asubuhi GMT.

Pambano hilo ni la kuwania taji la uzani wa kati ambalo kwa sasa linashikiliwa na Israel na pambano hilo litafanyika Sydney, Australia.

Hii si mara ya kwanza kwa Drake kuweka bet katika mechi mbali mbali lakini amekuwa akionesha Imani kubwa ya kuweka bet katika mchezo wa ndondi unaomhusisha Adesanya.

Itakumbukwa mwezi Aprili mwaka huu, Drake aliweka dau la £402,544 [$500,000] kwa Adesanya ili ashinde kwa njia yoyote ile lakini alifikiri wazi kwamba raia huyo wa New Zealand angemzuia mpinzani wake mkubwa na kuweka dau la £322,000 [$400,000] kwa ushindi wa KO.

Adesanya alishinda pambano hilo kumaanisha kuwa Drake aliondoka UFC 287 na kitita cha pauni milioni 2.19.

Je, Drake safari hii atakwenda nyumbani akifurahi ama Adesanya atamkosesha furaha?