logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Euro 2024: Lamine Yamal wa miaka 16 asaidia Uhispania kupiga Ufaransa na kutinga fainali

Baada ya kukamilika kwa mechi za nusu fainali leo, washindi watamenyana katika fainali itakayochezwa Jumapili, Julai 14.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo10 July 2024 - 04:49

Muhtasari


  • • Ufaransa walikuwa wameanza mechi vizuri sana huku mshambuliaji Kolo Muani akiwapatia bao la kwanza katika dakika ya 9.
  • •Mechi ya nusu fainali kati ya Uholanzi na Uingereza itachezwa mwendo wa saa nne usiku wa Jumatano.

Kinda wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16, Lamine Yamal alitunukiwa taji la mchezaji bora wa mechi huku Uhispania ikitoka nyuma na kuipiga Ufaransa katika mechi ya nusu fainali ya Euro 2024.

Washindi wa Kombe la Dunia 2018, Ufaransa walikuwa wameanza mechi vizuri sana huku mshambuliaji wa PSG Randal Kolo Muani akiwapatia bao la kwanza katika dakika ya 9.

Ilikuwa katika dakika ya 21 ambapo Lamine Yamal alipata nafasi, akaitumia vyema, na kufunga bao zuri lililompita kipa Mike Maignan wa Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 aliendelea kucheza mchezo wa kuvutia na alicheza jukumu kubwa katika bao la pili la Uhispania lililofungwa na Dani Olmo katika dakika ya 25.

Katika zaidi  ya dakika 65 zilizofuata za mechi hiyo ilikuwa pambano kubwa, huku timu zote zikijaribu kupata bao ili kuona nani atatinga fainali.

Licha ya nafasi nyingi zilizotengenezwa, si Uhispania wala Ufaransa waliofunga bao lingine hadi mwisho wa mechi iliyochezwa kwa dakika 90+5.

Uhispania sasa wanasubiri kujua watakutana na nani katika fainali ya michuano hiyo kati ya Uingereza na Uholanzi zinazocheza leo usiku, Julai 10.

Mechi ya nusu fainali kati ya Uholanzi na Uingereza itachezwa mwendo wa saa nne usiku wa Jumatano.

Baada ya kukamilika kwa mechi za nusu fainali leo, washindi wawili watamenyana katika fainali itakayochezwa Jumapili, Julai 14.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved