logo

NOW ON AIR

Listen in Live

FIFA yatoa orodha mpya ya timu bora za soka duniani, Uhispania yapanda hadi nafasi ya 3

Brazil imeshuka hadi nafasi ya tano baada ya kuonyesha viwango vya chini kwenye mashindanao ya Copa America.

image
na Davis Ojiambo

Michezo18 July 2024 - 12:21

Muhtasari


  • •Fifa imeorodhesha vilabu vya kitaifa  baada ya shughuli nyingi za soka kukamilika ikiwemo kombe la bara Ulaya na Copa America.
  • •Uingereza imeipiku Brazil walioonyesha viwango vya chini kwenye mashindano ya Copa America.

Mabingwa wapya wa bara Ulaya, Uhispania wamepanda hadi nafasi ya tatu katika viwango vya hivi punde vya FIFA vilivyochapishwa Alhamisi.

Washindi wa kombe la dunia 2022, Argentina wakishika nafasi ya kwanza kufuatia ushindi wao wa Copa America.

Viwango hivi vinakuja baada ya mwezi wa shughuli nyingi za soka, huku Argentina ikiishinda Colombia na kutwaa taji la Copa America na Uhispania ikiishinda Uingereza na kutwaa ubingwa wa Ulaya.

England ilipanda hadi nafasi ya nne, na kuruka Brazil ambao walionyesha viwango vya chini kwenye mashindano ya Copa America.Brazil walibanduliwa na Uruguay kwenye robo fainali baada ya mashuti ya penalti.

Kwingineko katika hatua ya 50 bora, timu mbili zimepanda daraja kwa njia ya kuvutia baada ya kutinga robo fainali ya mashindano yao ya bara.Uturuki imepanda  kutoka 42 hadi 26  na Venezuela  ikipanda hadi nafasi ya 37 kutoka 54.

New Zealand wamepanda hadi nafasi ya 94, wakirejea miongoni mwa 100 bora baada ya kushinda kombe la OFC.

  Tazama orodha ya kumi  bora:

    1. Argentina

    2 . Ufaransa

    3 .Uhispania

    4 . Uingereza

    5 . Brazil

    6 .Ubelgiji

    7.Uholanzi

    8 .Ureno

   9 .Kolombia

   10 . Italia


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved