logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyekuwa kocha wa Chelsea na Bayern, Thomas Tuchel ateuliwa kuwa meneja wa Uingereza

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 amesaini mkataba wa miezi 18 na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA).

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Football16 October 2024 - 07:31

Muhtasari


  • Uingereza imekuwa bila meneja wa kudumu tangu Gareth Southgate ajiuzulu kufuatia kushindwa kwa Three Lions kwenye fainali ya Euro 2024 dhidi ya Uhispania.
  • Utambulisho rasmi wa Tuchel unatarajiwa Jumatano Septemba 16, kwenye uwanja wa Wembley.

Kocha wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich Thomas Tuchel amekubali kuwa meneja ajaye wa timu ya taifa ya Uingereza almaarufu The Three Lions.

Ripoti kutoka Ujerumani zinaeleza kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 amesaini mkataba wa miezi 18 na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) - ambao utaanza Januari 1 mwaka ujao.

Tuchel atakuwa meneja wa tatu wa kudumu asiye Muingereza wa timu ya wanaume ya Uingereza baada ya Sven-Goran Eriksson na Fabio Capello.

Uingereza imekuwa bila meneja wa kudumu tangu Gareth Southgate ajiuzulu kufuatia kushindwa kwa Three Lions kwenye fainali ya Euro 2024 dhidi ya Uhispania mnamo Julai mwaka huu.

Kocha Lee Carsley, ambaye Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) lilimteua kwa muda, atasalia katika nafasi yake kwa mechi mbili za mwisho za Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Ugiriki na Jamhuri ya Ireland mnamo Novemba, huku Tuchel akitarajiwa kuchukua usukani rasmi baada ya hapo.

Utambulisho rasmi wa Tuchel unatarajiwa Jumatano Septemba 16, kwenye uwanja wa Wembley.

Tuchel anafahamu soka la Uingereza akiwa ameiongoza Chelsea kati ya Januari 2021 na Septemba 2022.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 51 alinyanyua kombe la Champions League, Fifa Club World Cup na Uefa Super Cup akiwa na The Blues kabla ya kutimuliwa.

Alishinda Kombe la Ujerumani akiwa na Dortmund na mataji mawili ya Ligue 1 akiwa na PSG, pamoja na mataji matatu ya nyumbani msimu wa 2019-20.

Kazi yake ya mwisho ilikuwa meneja wa Bayern lakini, baada ya klabu hiyo kushindwa kutwaa taji la Bundesliga kwa mara ya kwanza tangu 2011-12 msimu uliopita, aliiacha nafasi hiyo licha ya kuwa bado alikuwa na mwaka mmoja wa kumaliza mkataba wake.

Tuchel anatarajiwa kuhudumu kama kocha wa Uingereza hadi mwaka wa 2026.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved