Siku ya Jumanne, Oktoba 15, Klabu ya Soka ya Arsenal ilitangaza kuondoka kwa kocha wa timu ya wanawake Jonas Eidvall.
Katika
taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya klabu, Arsenal ilisema kuwa Jonas
aliondoka mara moja baada ya kujiuzulu.
"Tunaweza kuthibitisha kuwa Jonas Eidevall amejiuzulu wadhifa wake kama kocha mkuu wa kikosi cha kwanza cha wanawake na kutuacha mara moja," Arsenal ilisema.
Klabu hiyo yenye maskani yake jijini London ilitangaza zaidi kwamba Kocha Msaidizi wa kikosi cha kwanza cha wanawake Renée Slegers ataisimamia timu kama Kocha Mkuu wa Muda.
Huku akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal Edu Gaspar alitoa shukrani za klabu kwa kocha huyo na kusifu kazi yake.
"Tunamshukuru Jonas kwa kujitolea kwake kwa klabu na mafanikio yake hapa tangu ajiunge nasi mwaka wa 2021. Tunaheshimu sana kujitolea ambako alionyesha kwa kikosi cha kwanza cha wanawake na kutambua jukumu ambalo amecheza katika ukuaji na maendeleo ya timu ya wanawake ya Arsenal. Sote tunamtakia kila la kheri kwa siku zijazo,” Edu alisema.
"Lengo
letu sasa litageukia mchakato wa kuteua Kocha Mkuu mpya, na wakati huo huo,
kumuunga mkono Renée, anapochukua usukani wa timu kwa muda kuanzia na mechi
mbili muhimu wiki hii," aliongeza.
Jonas alijiunga na mnamo Arsenal Juni 2021 kutoka FC Rosengard ya Uswidi, na kushinda mataji mawili ya Kombe la Ligi ya Wanawake ya Continental Tyres League katika misimu mitatu kamili akiwa Arsenal.
Pia alisaidia timu hiyo kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya UEFA - mwaka wa 2022/23 - kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi.
Wanabunduki
pia wametangaza kuwa msako wa Kocha Mkuu mpya unaendelea na klabu itatoa
tangazo zaidi mchakato huo utakapokamilika.