Manchester United yaichapa Leipzig 5 kwa 0 kwenye UEFA

Muhtasari
  • Rashford aliwapa Mashetani Wekundu bao la mwisho na la ushindi katika njia ya uledi na kusaidia kikosi cha Solskjaer
  • Manchester United waliibuka washindi baada ya kuwalaza Leipzig mambao 5-0

Mchuano kati ya mashetani wekundu na Leipzig ilisubiriwa sana na mashabiki wa kandanda huku Man United wakiibuka washinda kwa kuwachapa RB Leipzig tano kwa nunge.

Bao la Mason Greenwood, hat-trick ya Marcus Rashford na mkwaju wa penalti wa Anthony Martial uliwatosha Mashetani Wekundu kuendeleza kampeni yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu bila kichapo.

Ni mechi ambayo ilianza timu zote zikiwa na matumaini ya juu huku matumaini ya Leipzig yakitulizwa baada ya dakika 21 hii ni baada ya Paul Pogba kushirikiana na Greenwood ambaye alifunga bao la kwanza la mechi hiyo.

Rashford alitambulishwa kwenye kipindi cha pili katika nafasi ya Donny van de Beek kwa dakika 68 na ilimchukua Muingereza huyo dakika sita pekee kucheka na wavu. 

Rashford aliongezea bao lingine la pili dakika nne baadaye huku Martial akitunukiwa matuta ya penalti na kuicharaza hadi kimyani na kufanya matokeo kuwa 4-0.

Rashford aliwapa Mashetani Wekundu bao la mwisho na la ushindi katika njia ya uledi na kusaidia kikosi cha Solskjaer kutamatisha mchezo huo kwa ushindi mkubwa wa 5-0.