Harambee stars watoka droo na timu ya Comoros

Muhtasari
  • Harambee stars wasalia katika nafasi ya pili katika mechi za Kundi G
  • Harambee stars watoka droo na timu ya Comoros
Image: Harambee stars

Mechi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika (AFCON) kati ya Kenya na Comoros ilitamatika droo ya 1-1 katika uwanja wa Kasarani.

Mechi hiyo ilimshuhudia Jacob 'Ghost'Mulee akirejea uwanjani baada ya kuteuliwa kwa mara ya pili kuwa kocha mkuu wa Stars. Mulee alimrithi Francis Kimanzi ambaye alijiuzulu mnamo Jumatano, Oktoba 21.

Licha ya kutawala dakika za mapema za mchuano huo, Comoros ndio walijiweka kifua mbele katika dakika ya 26 ya mchezo kupitia kwa Bakari Said kwa kufungua kwa bao moja.

Hata hivyo, wageni walipata pigo kubwa katika dakika ya 41, baada ya Youssouf M'Changama kulishwa kadi nyekundu.

Les Coelacantes walifaulu kujitetea mechi nzima na kuzoa pointi moja ugenini huku mechi hiyo ikitamatika sare ya 1-1.

Harambee Stars sasa wamesajili droo tatu katika mechi za Kundi G za kufuzu kwa AFCON kutoka kwa michezo mbili za awali.

Stars wanasalia kwenye nafasi ya pili katika kundi hilo huku Comoros wakiongoza na pointi tano.