- " Mimi ni mwanamme mweusi na kila siku nina fahari ya kujiita hivyo’ amesema katika twitter
- Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyepewa tuzo ya MBE kwa kazi yake kupambana na umaskini wa chakula miongoni ma watoto ,alipokea jumbe za kumbagua rangi yake jumamosi usiku baada ya kilabu yake kutoka sare tasa na Arsenal
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford amesema amepitia ‘ukatili mkubwa Zaidi wa kibinadamu’ baada ya kutukunawa kwa msingi wa rangi yake katika mitandao ya kijamii siku ya jumaksi usiku .
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyepewa tuzo ya MBE kwa kazi yake kupambana na umaskini wa chakula miongoni ma watoto ,alipokea jumbe za kumbagua rangi yake jumamosi usiku baada ya kilabu yake kutoka sare tasa na Arsenal
" Mimi ni mwanamme mweusi na kila siku nina fahari ya kujiita hivyo’ amesema katika twitter
" Hakuna yeyote ,au tamko lolote litakalonifanya nijihisi kivingine . kwa hiyo pole sana iwapo ulifikiri kwamba jibu langu litakuwa na machungu , hutalipata jibu kama hilo hapa’ ameongeza Rashford .
Akizungumza katika kipindi cha Match of the Day, aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal na England Ian Wright amesema maamlaka na kampuni za mitandao ya kijamii zinafaa kuchukua hatua Zaidi kukabiliana na wanaoendeleza ubaguzi kama huo mitandaoni
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Tottenham, Newcastle na England Jermaine Jenas aliongeza : "kumbi hizi ,nazihitaji zinionyeshe watu hawa na kutoa hakikisho kwamba hatua zinachukuliwa ili kupata haki ,kwa wale ambao wanauliza mbona bado tunapiga goti ,jibu ndilo hilo’
Shirikisho la soka la FA limeelezea kujitolea kwake katika kupambana na wanaoendeleza ubaguzi wa rangi