Harambee Stars yailaza Togo mabao 2 kwa 1

Muhtasari
  • Harambee Stars yailaza Togo kwa mabao 2 kwa 1
  • Matokeo hayo yana maana kuwa Misri na Comoros watashiriki raundi nyingine ya mtanange huo licha ya matokeo ya Togo
Image: Harambee Stars

Harambee Stars wamemaliza kampeni yao ya kuingia kwenye mchuano wa Kombe la Afrika (AFCON)baada ya kupiga Togo 2-1 na kumaliza watatu Kundini G.

Ni mechi ambayo ilishuhudia harambe stars kuwa washindi siku ya Jumatatu.

Stars walifanya ziara nchini Togo na droo ya 1-1 dhidi ya Misri waliopata kwenye mechi kali iliyoandaliwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Kasarani.

Matokeo hayo yana maana kuwa Misri na Comoros watashiriki raundi nyingine ya mtanange huo licha ya matokeo ya Togo.

Image: Harambee Stars

Lakini hayo hayakuwazuia stars kurekodi matokeo mazuri nyumbani huku Hassan Abdallah akionja wavu wa Sparrowhawks.

Staa huyo wa Bandari alifungua ukurasa wa mabao punde baada ya muda wa mapumziko kabla ya Masud Juma kusawazisha katika dakia ya 65.

Juhudi za wenyeji kupata bao la kufutia machozi zilizaa matunda kupitia kwa Henri Eninful ambaye alifanya mambo kuwa 2-1.