Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 01.07.2021: Sancho, Rice, Kane, Sterling, Haaland, Mbappe

Sancho atapatiwa jezi nambari saba katika klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa inavaliwa na mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani,

Muhtasari

•Manchester City ina mpango wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa England Raheem Sterling kuhusu hatma yake , huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza..

•Tottenham imemuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo kuwa mkufunzi mpya kwa kandarasi ya miaka miwili .

Jadon Sancho na Marcos Rashford wa Uingereza
Jadon Sancho na Marcos Rashford wa Uingereza
Image: Hisani

Huku makubaliano ya kumsaini winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho yakiafikiwa , kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice ,22, beki wa Villareal mwenye umri wa miaka 24 Pau Torres na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane 27 , ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer (Guardian)

Sancho atapatiwa jezi nambari saba katika klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa inavaliwa na mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34. (Metro)

Mshambulizi wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho
Mshambulizi wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho
Image: Hisani

United pia ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Leon Goretzka, 26, ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika 2022.. (Bild - in German)

Hata hivyo , United na Liverpool huenda wakamkosa winga wa Ufaransa Kingsley Coman baada ya Bayern Munich kusema kwamba anaweza kuuzwa kwa bei ya £77m. (Bild)

Tottenham imemuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo kuwa mkufunzi mpya kwa kandarasi ya miaka miwili .

Nuno aliondoka Wolves mnamo mwezi Mei baada ya misimu minne ambapo alionesha umahiri wake wa kazi hiyo ambapo alifanikiwa kuipandisha klabu hiyo kutoka ligi ya mabingwa hadi kufuzu robo fainali ya kombe la Europa.

Kocha mpya wa Tottenham, Nuno Espirito Santo
Kocha mpya wa Tottenham, Nuno Espirito Santo
Image: Hisani

Manchester City ina mpango wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa England Raheem Sterling kuhusu hatma yake , huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza.. (Mail)

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amechukua nafasi ya mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Leonardo katika mazungumzo ya kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 inakamilika 2022.. (L'Equipe, via Get French Football News)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ana Imani kwamba The Blues inaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, mwisho wa msimu huu . (Express)

Mchezaji wa timu ya Portugal ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Nuno Tavares, 21, atafanyiwa uchunguzi wa matibabu katika klabu ya Arsenal kabla ya kujiunga na The Gunners kwa dau la £7m kutoka Benfica. (Goal)

Nuno Tavares wa Benfica
Nuno Tavares wa Benfica
Image: Hisani

Chelsea wamewasilisha ombi la mwisho kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Lauren James, 19, dadake beki wa Blues Reece James. (Goal)

Leicester inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan katika kinyang'aanyiro cha kumsaini winga wa Itali na Sassuolo Domenico Berardi, 26, ambaye amewavutia the Azzurri katika michuano ya 2020. (Corriere dello Sport - in Italian)

Newcastle United wamewasilisha ombi la £1.5m kumnunua beki wa Wolves Dion Sanderson huku wakishindana na Sunderland kumsaini mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 21 (Mail)

Klabu ya RB Leipzig itamuwacha kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu kwa bei ya chini huku Arsenal, AC Milan na Roma zote zikimuwania kiungo huyo mchezeshaji mwenye urmi wa miaka 27.. (Bild - in German)

Nahodha wa klabu ya Rangers James Tavernier ananyatiwa na Manchester United, Brighton, Norwich na Arsenal. Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 alitia saini kandarasi mpya mwezi Aprili , inayomfanya kusalia katika klabu hiyo hadi 2024. (90min)

(Maongezi:Samuel Maina)