Crystal Palace yamteua aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, Patrick Viera kama meneja.

Viera, 45, ambaye ni mzaliwa wa Dakar, Senegal ametia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya London.

Muhtasari

•Kabla ya kujiunga na Palace, Viera amekuwa  kocha katika timu mbili, New York City F.C ya Marekani na Nice ya Ufaransa.

•Viera ni miongoni mwa wachezaji wa awali ambao wanaheshimika sana haswa na mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya kuichezea mechi 279 na kufunga mabao 29 kati ya mwaka wa 1996 na 2005

Patrick Viera
Patrick Viera
Image: Twitter

Klabu ya Crystal Palace imemteua aliyekuwa mchezaji wa Arsenal, Patrick Viera kama meneja .

Viera, 45,  ambaye ni mzaliwa wa Dakar, Senegal ametia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya London.

Kabla ya kujiunga na Palace, Viera amekuwa  kocha katika timu mbili, New York City F.C ya Marekani na Nice ya Ufaransa.

Familia ya Viera ilihamia nchini Ufaransa akiwa na miaka 8 na akaanza kucheza soka akiwa huko hadi kufikia kiwango cha kuchezea timu ya taifa hilo.

Viera ni miongoni mwa wachezaji wa awali ambao wanaheshimika sana haswa na mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya kuichezea mechi 279 na kufunga mabao 29 kati ya mwaka wa 1996 na 2005. 

Alisaidia Arsenal kushinda ligi mara tatu, 1997/98, 2002/03 na 2003/04. Alikuwa nahodha kwenye klabu hiyo kati ya mwaka wa 2002 na 2004.

Kando na Arsenal, Viera alichezea Cannes ya Ufaransa, Inter Milan na Juventus za Italia na Manchester City ya Uingereza.

Baada ya kukamilisha taaluma yake ya kucheza kandanda akiwa Manchester City, alianza kufunza chuo cha kufunza kandanda cha klabu hiyo kabla ya kuelekea Marekani kufunza New York City F.C.