•Klabu ya Everton nchini Uingereza imemsimamisha kazi mchezaji mmoja wa kikosi cha kwanza ili kupatia nafasi uchunguzi wa polisi kuhusiana na tuhuma dhidi yake kuendelea.
•Hata hivyo hawakutaja mchezaji mhusika wala kesi inayomkabili
Klabu ya Everton nchini Uingereza imemsimamisha kazi mchezaji mmoja wa kikosi cha kwanza ili kupatia nafasi uchunguzi wa polisi kuhusiana na tuhuma dhidi yake kuendelea.
Kupitia tovuti yake rasmi, klabu hiyo ilitangaza kuwa wataendelea kushirikiana na maafisa wa usalama katika uchunguzi wao.
Hata hivyo hawakutaja mchezaji mhusika wala kesi inayomkabili.
"Klabu itaendelea kusaidia maafisa wa usalama katika uchunguzi wao na hakuna ujumbe mwingine utatolewa kwa sasa" Everton iliandika.
Wiki chache zilizopita klabu hiyo ilimteua aliyekuwa kocha wa Liverpool Rafa Benitez kama kocha mkuu baada ya kuondoka kwa Carlo Ancelloti kuelekea Real Madrid mapema mwezi huo.
Everton ilimaliza katika nafasi ya kumi msimu uliopita na kuzoa alama 59.