Mfahamu nyota wa soka Christiano Ronaldo; Uwanjani yumo na kwa wanawake yumo

Zipo tafiti na machapisho mengi yanaokinzana kuhusu historia ya Ronaldo lakini mengi yanakubaliaa kwamba, nyota huyo wa kiataifa wa Ureno ana asili ya Afrika Magharibi

Muhtasari

•Ukitaja wanasoka mahiri wawili wa kizazi cha sasa duniani, jina la Cristiano Ronaldo lazima liwepo kwenye orodha hiyo, ama litakuwa la kwanza ama la pili, inategemea na tafsiri ya anayeweka orodha hiyo kati yake na Lionel Messi.

•Ronaldo ana watoto wanne, wa kwanza ni Cristiano Jr. aliyezaliwa Juni 17 2010 huko Marekani kwa mama ambaye, amefichwa utambulisho wake kwa mkataba.

Image: REUTERS

Ukitaja wanasoka mahiri wawili wa kizazi cha sasa duniani, jina la Cristiano Ronaldo lazima liwepo kwenye orodha hiyo, ama litakuwa la kwanza ama la pili, inategemea na tafsiri ya anayeweka orodha hiyo kati yake na Lionel Messi.

Na ukiongoeza orodha hiyo na kufikia wachezaji wanne wakali waliowahi kutokea duniani, jina lake litakuwepo tu itategemea utawaorodheshaje kati yake na Messi, Edson Pele na Diego Maradona.

Hilo linakuonyesha isivyo shaka kuhusu ubira wake ndani ya uwanja akiwa na klabu yake ama timu yake ya taifa.

Amecheza Ureno kwenye Klabu ya Lisbon, Uingereza kwenye klabu ya Manchester United, Uhispania kwenye Real Madrid na sasa anakipigia Klabu ya Juventus.

Jina la 'Ronaldo' na historia yake

 

Ronaldo akiwa na mama yake (aliyekaa) na dada zake
Ronaldo akiwa na mama yake (aliyekaa) na dada zake
Image: HISANI

Wengi hasa wafuatiliaji wa soka katika miaka ya 1990s mpaka 2000s wanamfahamu mtu anaitwa Ronaldo Luís Nazário de Lima, alikuwa maarufu kwa jina la Ronaldo, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Inter Milan, Barcelona, Real Madrid, PSV, Corinthians na timu ya taifa ya Brazili ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara mkubwa na mmiliki wa timu ya Laliga ya Real Valladolid.

Alikuwa mshambuliaji mahiri akitwaa kombe la dunia na Brazil mwaka 2002 na kutwa a tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 3. Wengi wanadhani jina la Ronaldo wa sasa limetokana na umaarufu wa Ronaldo wa zamani, la hasha Ronaldo wa sasa jina lake lina historia tofauti.

Cristiano Ronaldo Dos Santos Aveiro alizaliwa mwaka Februari 5, mwaka 1985 huko Funchal katika visiwa vya Madeira, kwa mama Maria Doroles Dos Santos Aveiro na marehemu baba yake Jose Dinis Aveiro.

Ronaldo (kushoto0 akiwa na baba yake Jose Dinis Aveiro
Ronaldo (kushoto0 akiwa na baba yake Jose Dinis Aveiro
Image: HISANI

Alipozaliwa tu baba yake akampatia jina la Ronaldo akimuona kama Ronald Regan (Rais wa Marekani) ajae.

Wakati huo baba yake hakuwa na wazo kabisa kuhusu mwanae kuwa mwanasoka, alimpenda sana Rais Regan, ambaye wakati Ronaldo anazaliwa ndio alikuwa ametoka kuapishwa kuwa rais katika awamu yake ya pili ya uongozi

Maisha ya utotoni ya Ronaldo

Image: GOOGLE

Ronaldo ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watatu waliozaliwa na wazazi wake, mwingine ni Maria Dolores mwenye fani ya upishi na Jose Denis Aveiro ambaye ni askari wa zamani, mtunza bustani na mtunza vifaa. Ana ndugu wengine wakubwa kaka yake Hugo, na dada zake wawili Elma na Liliana Cátia "Katia".

Katika utoto wake, Ronaldo alikuwa anadekezwa na kudeka kupita kiasi. Kuna wakati ndugu zake hasa kaka zake walilazimika kubeba makosa yake. Alijiliza na kujilalamisha kitoto kila alipoona amekosea, na kwa huruma zao nudu zake wakubwa walibeba makosa yake mbele ya wazazi wao.

Baba yake José, alifariki mwaka 2005 Ronaldo akiwa na miaka 20 tu, huku mama yake akitibiwa saratani ya matiti mwaka 2007, ingawa anaendelea vyema sasa.

Kama si daktari almanusura mama yake aitoe mimba yake

Mama yake Ronaldo Maria Doroles Aveiro akiwa na wajukuu zake
Mama yake Ronaldo Maria Doroles Aveiro akiwa na wajukuu zake
Image: HISANI

Wazazi wa Ronaldo walikuwa masikini wasijiweza, ingawa walijitahidi kati ya wtoto wote kumpa kila alichokitaka Ronaldo kama kitinda mimba. Ronaldo hakuwah kukosa ngo ya aina yoyote aliyohitaji hata kama itawalazimu wazazi wake kukopa. Alipendwa sana na kila mwanafamilia kwa sababu ya uchangamfu wake na namna alivyojipenda yeye mwenyewe.

Kutokana na umasikini, mama yake alipopata mimba ya Ronaldo aliwaza kuitoa. Mama yake aliwahi kukiri kwamba umasikini, ulevi wa baba yeke na ukubwa wa familia yake iliyokuwa tayari ina watoto wengine wengi zilizkuwa sababu za kutaka kutoa mimba hiyo.

Kama si daktari aliyemuhudumia wakati huo leo soka lisingekuwa na Ronaldo na lisingekuwa na mfungaji mahiri wa aina yake.

Daktari alikataa kuitoa mimba hiyo, kwa sababu za kiafya, licha ya kukubaliana naye kuhusu hali ngumu ya maisha ya familia ya Ronaldo, ambayo walilazimika watoto wote kulala katika chumba kimoja.

Baada ya daktari kukataa wazo la Maria Doroles Aveiro la kutoa mimba, mama huyo ilibidi atafute njia mbadala, akaanza kunywa pombe mpaka anakuwa hoi na kukimbia kupitia kiasi akitumaini mimba hiyo ingetoka, lakini haikuwezekana na mwishowe akaamua kuzaa tu.

Ronaldo ni muafrika?

Image: GETTY IMAGES

Zipo tafiti na machapisho mengi yanaokinzana kuhusu historia ya Ronaldo lakini mengi yanakubaliaa kwamba, nyota huyo wa kiataifa wa Ureno ana asili ya Afrika Magharibi. Kwanini wanasema hivyo? Ni kwa sababu babu yake ana asili ya Praia, Cape verve, moja ya visiwa maarufu Afrika.

Kizazi cha kwanza cha Ronaldo cha Isabel Rosa da Piedade(babu na bibi zake) walizaliwa na kuishi Praia, kizazi kilichofuata cha Cirilo Aveiro ambaye ni babu wa baba yeke kikiwa na miaka 16 walikimbilia kisiwa cha Medeira, na hapo vikafuata vizazi vitatu mpaka cha Ronaldo.

Kwa sababu ya asili hiyo, waafrika hasa wa Cape Verde wanamuona ni ndugu yao wa damu, licha ya kuwa na uraia wa ureno kutokana na kuzaliwa kwa baba na babu waliokuwa na urai wan chi hiyo.

Akiwa na miaka 12 aachana na wazazi wake na kutimkia Lisbon

Ronaldo aliondoka nyumbani akiwa na miaka 12 kwenda kusaka maisha ya soka
Ronaldo aliondoka nyumbani akiwa na miaka 12 kwenda kusaka maisha ya soka
Image: GETTY IMAGES

Ronaldo alianza kuonyesha kupenda soka toka akiwa na umri mdogo kabisa, na baba yake alianza kuona hilo na kuanza kumpeleka viwanjani. Licha ya kuanza shule lakini hakuwa na mpango na shule na mara kadhaa alikacha masomo na kumsindikiza baba yake kwenye klabu ya Andorihna huko Funchal, aliyekuwa mtunza vifaa wa timu. Alipotimiza miaka 8 akasainiwa timu ya watoto ya klabu hiyo.

Katika kumsaidia zaidi, baba yake Jose Aveiro akaamua kuacha kazi katika timu ya wakubwa na kuwa mtunza vifaa wa timu ya watoto, ili kuwa karibu na mwanae na kumsaidia kukua katika soka.

Mchezaji mwenzake wa Andorinha wakati huo wakiwa wadogo, ambaye kwa sasa ni kocha akionoa mpaka Andorihna yenyewe, Ricardo Santos, aliwahi kunukuliwa akisemema 'C. Ronaldo alikuwa anapenda kushinda, ikitokea timu imefungwa, analia sana, alikuwa analia sana mpaka akapachikwa jina la mtoto mlizi',.

Akiwa na miaka 12 , akaondoka Medeira na kwenda Lisbon kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kisoka akiwaacha wazazi wake. Akafanya mjaribio ya siku 3 katika timu ya watoto ya Sporting Lisbon na kufaulu na kusajili kwa Pauni 1,500 tu ilikuwa mwaka 1997.

Upweke katika jiji la Lisbon ulimliza kila leo 'mtoto mlizi', lakini alijiambia anapaswa kupambana kusaidia kuondoa umasikini wa wazazi wake

Matatizo ya Moyo na tishio la kuacha soka

Akiwa Sporting Lisbon, alianza kuonyesha dalili za kuwa na matatizo ya moyo. Hakuwa sawa, na kuna wakati moyo wake ulionekana kushindwa kufanya kazi sawa sawa. Madakatari wa Klabu hiyo ilibidi waombe ruhusa kwa wazazi wake ili kumfanyia upasuaji, kwa sababu bila kufanya hivyo soka angelisikia kwenye redio.

Damu ilikuwa haitembei vizuri mwilini kwa msukumo wa moyo uliokuwa na shida. Wazazi wake walifarijika na hilo, matibabu yalifanyika na kufanikiwa kurejea uwanjani.

Safari yake ya kuwa maarufu na mchezaji bora duniani

Safari ya Ronaldo kisoka ilikuwa ya milima na mabonde, lakini akapata mteremko akiwa Lisbon
Safari ya Ronaldo kisoka ilikuwa ya milima na mabonde, lakini akapata mteremko akiwa Lisbon
Image: HISANI

Ronaldo alikuwa mchezaji muhimu katika timu ya vijana ya Sportin Lisbon ya Ureno, lakini safari yake ilianza vyema baada ya kocha wa timu ya wakubwa, Laszlo Boloni kumpa nafasi wakati wa mechi za kujiandaa na msimu. Na katika moja ya mechi za kirafiki kati ya timu hiyo na Manchester United, iliyopigwa Agosti 6, 2003 akiwa na miaka chini ya 18, Ronaldo alicheza soka la uhakiwa pamoja na umri wake mdogo na kuwafanya wachezaji wakonge wa Manchster wakati huo kumuomba kocha Sir Alex Fergison kumsajili haraka.

'Tulikuwa kwenye basi tunamsubiri mtendaji mkuu David Gill na meneja Ferguson, tulisukuma asainiwe, na ndani ya wiki moja alikuwa mchezaji wa Manchester United', alisema Rio Ferdinand, beki wa zamani wa Manchester.

'Kila kitu kilenda haraka sana, siku mbli baadae nilizungumza na kocha wakanipekea England, Manchester nikasajiliwa', alisema Ronaldo kwenye moja ya mahojiano yake.

Beki mwingine Mikael Silvester aliwahi kunukuliwa akisema ; alicheza kwa kiwango cha juu siku hiyo, kabla ya mchezo kuanza hakuna aliyekuwa anamjua, lakini baada ya mchezo kila mtu alimjua', alisema kuhusu mechi hiyo ambayo Manchester ililala kwa mabao 3-1.

Licha ya kwamba alishafanya mazungumzo na Arsen Wenger kwa ajili ya kujiunga na Arsenal, Manchester walimsajili haraka na kwenda kuwa mchezaji mkubwa duniani. Katika miaka 6 aliyokuwa Manchester alishinda mataji matatu ya ligi kuu na moja la klabu bingwa Ulaya huku akiifungia mabao 118.

Akaenda Real Madrid kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa pauni 80mil, akiwa pale akashinda karibu kila kitu kitu ikiwemo mataji mawili ya laliga na manne ya ligi ya mabingwa Ulaya, kabla ya kutimikia Juventus mwaka 2018 ambapo ameshinda mataji kadhaa yakiwemo mawili ya Seria A.

Tuzo, mafanikio, utajiri na mtindo wa maisha

Ronaldo akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa dunia
Ronaldo akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa dunia
Image: HISANI

Ukiacha makombe lukuki aliyoyazoa akiwa na vilabu vya Manchester United, Real Madrid na sasa Juventus, Ronaldo ana tuzo binafsi zaidi ya 40 kutokana na mchango wake kwenye timu alizowahi kuchezea, ikiwemo tuzo ya mwanasoka bora wa dunia 'Ballon dor aliyetwaa mara tano , mara moja nyuma ya Lionel Messi.

Amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake ya taifa ya Ureno, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo kwa mabao yake 109 akiipa pia taji la Euro mwaka 2016. Mbayo yake matano katika michuano ya Euro 2020 yamemfanya kufikisha mabao 109 akiwa na timu ya taifa 109 na umfikia Ali Daei wa Iran aliyekuwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi ya timu ya taifa duniani.

Ronaldo pia ndiye mfungaji bora wa muda wote wa michuano ya Ulaya akiwa na mabao 14 akimpiku Michel Platin mwenye mabao 9 na Antoine Griezmann mwenye 7.

Mafanikio makubwa aliyapata zaidi akiwa na klabu yake ya Real Madridi alipoipachikia mabao 450 katika michezo 438. Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza anayeendelea kucheza kuingiza zaidi ya dola $bilioni 1 katika maisha yake ya soka huku mkataba wake wa miaka minne na Juventus unaomalizika mwaka 2022 ukimuingizia wastani wa $64milioni.

Ronaldo ni miongoni mwa wanamichezo matajiri duniani
Ronaldo ni miongoni mwa wanamichezo matajiri duniani
Image: HISANI

Ronaldo si mtu wa kujikweza sana, lakini mtindo wake wa maisha unamtofautisha kiasi na mastaa wengine duniani. Ana wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii, akifikisha wafuasi 500milioni kwenye mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter.

Hana Tatoo mwilini mwake kama watu wengine maarufu na amekuwa akipenda sana kuchangia damu. Pia Si mtu wa starehe za pombe ama kwenda kwenye majumba ya starehe sana, lakini amekuwa na mahusiano mengi, mtaani unaweza kumwita ni mtu wa 'totoz'.

Ronaldo na mabinti damu damu

Ronaldo na mpenzi wake Georgina
Ronaldo na mpenzi wake Georgina
Image: HISANI

Ronaldo ana watoto wanne, wa kwanza ni Cristiano Jr. aliyezaliwa Juni 17 2010 huko Marekani kwa mama ambaye, amefichwa utambulisho wake kwa mkataba.

Januari 2015, Ronaldo alieleza umma uhusiano wake wa miaka mitano na mwaamitindo wa Urusi Irina Shayk ulikoma. Kwa sasa ana uhusiano na mrembo mwingine wa Hispania Georgina Rodríguez, muuza duka msaidizi wa zamani ambaye wamefanikiwa kuzaa binti yake wa mwisho Alana Martina, aliyezaliwa Novemba 12 2017.

Ingawa ana mapacha wengine, mmoja wa kike mmoja wa kiume, Ronaldo amekuwa mwingi wa habari kwa mabinti, akiwa na mahusiano na mabinti mabalimbali ambao wengi wao ni warembo na wanamintindo.

Ronaldo na mpenzi wake wa zamani Irina Shayk
Ronaldo na mpenzi wake wa zamani Irina Shayk
Image: HISANI

Inatajwa mpaka mwaka huu, amewahi kuwa na uhusiano na mabinti 31 tofauti tofauti katika maisha yake, ambao wengi kati yao wanafahamika na maarufu, ingawa wapo ambao hawafahamiki na pengine yeye kutowafahamu kwa majina.

Baadhi ya wapenzi wake ni Merche Romero, Nereida Gallardo, Kim Kardashian, Irina Shayk, Rita Pereira, Andressa Urach na Georgina Rodriguez.

Inaelezwa kuwa uhusiano wa kukutana na mtu kwa ahadi ya kufanya tendo la ndoa tu na kuachana kila mtu kivyake, umemuingiza katika makubaliano ya siri. Mtoto wake wa kwanza Ronaldo Jr, mama yake ambaye hajulikani, ameingia mkataba na Ronaldo wa kutojitambulisha kuhusu mtoto huyo na kukaa naye mbali. Mtoto huyo kalelewa na bibi yake ambaye ni mama yake na Ronaldo.

Ronaldo na urafiki wa kweli kwa Alberto Fantrau

Ronaldo (kushoto) na rafiki yake Alberto
Ronaldo (kushoto) na rafiki yake Alberto
Image: GOOGLE

Urafiki wawawili hawa ulijulikana kwenye moja ya matukio ya Ronaldo kupokea tuzo aliposema ' Kweli mimi ni mchezaji bora na mafanikio haya yote ni kwa sababu ya moyo mzuri wa rafiki yangu akimuonyeshea Fantrau.

Ronaldo aliendelea kusema ' tulikuwa tunacheza pamoja timu ya watoto mtaani, walipokuja wasaka vipaji wa Sporting Lisbon kutuangalia walitueleza, mshambuliaji atakayefunga mabao mengi atakwenda Spots Academy, ambayo ni hatua muhimu ya kuelekea timu ya wakubwa na kukua kisoka. Siku hiyo tulishinda mabao 3-0. Nilifunga goli la kwanza, Alberto akafunga la pili, lakini goli la tatu ndilo lililoleta mvuto zaidi. Alberto alibaki yeye na kipa tu akampiga chenga kipa kilichobaki ilikua kufunga goli lililokuwa wazi. Wakati huo nilikuwa nakimbia upande wake, sasa badala ya kupiga na kufunga akanipasia mie nikafunga, na hiyo ndio sababu nipo hapa leo'.

Lakini baada ya mechi kumalizika nilimuuliza 'Kwanini ulifanya vile? Akajibu ' kwa sababu najua kwamba wewe ni mchezaji mzuri kuliko mie na utafika mbali kwenye soka, ulihitaji kupewa msaada ule',

Mpaka leo watu hawa ni mrafiki wa kutupwa, wasioachana licha ya mara kadhaa kutengenishwa na majukumu yao.

Afungua jumba lake la makumbukumbu la 'The Muse CR7'

 

Jumba la Makumbusho la CR7, kila anayekwenda kwenye jumba hilo hulipa euro 5, huku wanafunzi na watoto chini ya miaka 10 wakiingia bure.
Jumba la Makumbusho la CR7, kila anayekwenda kwenye jumba hilo hulipa euro 5, huku wanafunzi na watoto chini ya miaka 10 wakiingia bure.
Image: HISANI

Mafanikio yake na tuzo alizotwaa yamemfanya kuanzisha jumba la kumbukumbu lililoko huko alikozaliwa Funchal Madeira linalosimamiwa na kaka yake. Juu ya jumba hilo la makumbusho kuna hotel yake maarufu aliyoianzisha kwa kushirikana na Pestana Group.

Nje ya jumba hilo kuna sanamu lake na nembo kubwa ya CR7, C ikisimama kwa jina lake Cristiano, R ni Ronaldo na 7 ni namba ya jezi iliyompa umaarufu akiwa na Manchester United na Ureno.

Pestana CR7 ni hotel maarufu kwwenye eneo alikozalliwa Ronaldo la Medeira
Pestana CR7 ni hotel maarufu kwwenye eneo alikozalliwa Ronaldo la Medeira
Image: HISANI

Mbali na historia ya gwiji hili utakayoipata kwenye jumba hilo, pia tuzo na makombe yote 126 aliyoshinda binafsi na timuzake utayapata. Limepambwa na nakshi za picha zake, akiwa na jezi za timu mbalimbali alizochezea. Jumba hili la makumbusho lenye ukubwa wa mita za mraba 400 alikuwa analisimamia kaka yake, Hugo Dinarte Aveiro.