Niko katika timu inayoweza kushinda taji la klabu bingwa- Lionel Messi

PSG bado inatafuta taji lao la kwanza katika mashindano hayo , baada ya kupoteza kwa Bayern katika fainali ya 2020.

Muhtasari

•Nahodha huyo wa timu ya Argentina ,34 alishinda mataji manne ya kombe la klabu bingwa na Barcelona , mara ya mwisho ikiwa 2015.

•Kuwasili kwa Messi katika mji mkuu wa Ufaransa kunakamilisha mojawapo ya safu kali ya mashambulizi katika historia.

Image: GETTY IMAGES

Lionel Messi amesema kwamba ana ndoto ya kushinda taji la klabu bingwa Ulaya zaidi baada ya kujiunga na PSG , akiongezea kwamba: Nadhani tuna timu ya kuweza kushinda.

Nahodha huyo wa timu ya Argentina ,34 alishinda mataji manne ya kombe la klabu bingwa na Barcelona , mara ya mwisho ikiwa 2015.

PSG bado inatafuta taji lao la kwanza katika mashindano hayo , baada ya kupoteza kwa Bayern katika fainali ya 2020.

''Lengo langu na ndoto yangu ni kushinda taji la klabu bingwa mara moja zaidi'' , Messi alisema wakati wa uzinduzi wake kama mchezaji wa PSG.

Messi aliondoka Barcelona – ambayo alijiunga nayo akiwa na umri wa miaka 13 – baada ya kushindwa kupata mkataba mpya chini ya sheria za Fair play za ligi ya la liga.

Akitambuliwa kama mchezaji bora wa wakati wote, alifunga magoli 672 katika mechi 778 akiwachezea mabingwa hao wa Catalan.

Alitia saini kandarasi ya miaka miwili kujiunga baada ya kuondoka Barcelona.

Kuwasili kwa Messi katika mji mkuu wa Ufaransa kunakamilisha mojawapo ya safu kali ya mashambulizi katika historia.

Raia huyo wa Amerika kusini anatarajiwa kucheza katika safu ya mashambulizi pamoja na Neymar na Kylian Mbappe.

Rais wa PSG Nasser Al.-Khelaifi anaamini kwamba usajili wa Messi utachangia kumshawishi Mbappe ambaye kandarasi yake inakamilika 2022 kusalia katika klabu hiyo.