Beki wa Manchester City Benjamin Mendy ashitakiwa kwa ubakaji

Makosa hayo yanawahusu walalamikaji watatu walio na umri wa zaidi ya miaka 16 na yanaelezwa kufanyika kati ya Oktoba 2020 na Agosti mwaka huu

Muhtasari

•Mendy, anayeishi eneo la Prestbury, kwa sasa anashikiliwa na polisi kabla ya kufikishwa mahakamani leo katika mkoa ya Chester.

•Manchester City ilisema mlinzi huyo, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Ufaransa , ameondolewa kwenye kikosi hicho mpaka baada ya uchunguzi wa kesi yake hiyo.

Image: PA MEDIA

Mlinzi wa Manchester City, Benjamin Mendy (27) ameshitakiwa kwa makosa manne ya ubakaji na lingine la unyanyasaji wa kijinsia, kwa mujibu wa Polisi wa Cheshire.

Makosa hayo yanawahusu walalamikaji watatu walio na umri wa zaidi ya miaka 16 na yanaelezwa kufanyika kati ya Oktoba 2020 na Agosti mwaka huu.

Mendy, anayeishi eneo la Prestbury, kwa sasa anashikiliwa na polisi kabla ya kufikishwa mahakamani leo katika mkoa ya Chester.

Mlinzi huyo wa kushoto amekuwa akiwachezea mabingwa hao wa ligi kuu England msimu uliopita tangu mwaka 2017 alipojiunga nao akitokea Monaco kwa ada inayoripotiwa kuwa ni £52m.

Msemaji wa Polisi alisema: "Polisi Cheshire na kitengo cha mashataka cha Crown wanapenda kuwakumbusha kuwa kesi ya jinai inayomkabili Mendy ipo na ana haki zote za kusikilizwa."

Manchester City ilisema mlinzi huyo, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Ufaransa , ameondolewa kwenye kikosi hicho mpaka baada ya uchunguzi wa kesi yake hiyo.

"Suala hilo liko kwenye mchakato ya kisheria kwa hivyo klabu haitaweza kuzungumzia zaidi mpaka litakapokamilika," Klabu hiyo iliongoeza.