Cristiano Ronaldo avunja rekodi ya kimataifa ya ufungaji wa magoli

Ronaldo yuko juu kwa magoli 111 na Daei anafuatia kwa magoli 109, kwa hilo hapana shaka.

Muhtasari

•Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 alifunga magoli mawili kunako dakika za mwisho za mchezo-na hivyo kuvunja rekodi na kuipita baada ya kupiga mkwaju wa penalti uliyookolewa na Gavin Bazunu.

•Ronaldo, ambaye alijiunga na Manchester United kutoka Juventus msimu huu katika siku ya mwisho , na , Daei ni wachezaji pekee wa kiume kuwahi kufunga mabao 90 au magoli mengi ya kimataifa.

Cristiano Ronaldo ameifungia magoli 28 Ureno kwa kichwa 28 , yakiwemo magoli mawili dhidi ya Jamuhuri ya Ireland.
Cristiano Ronaldo ameifungia magoli 28 Ureno kwa kichwa 28 , yakiwemo magoli mawili dhidi ya Jamuhuri ya Ireland.
Image: GETTY IMAGES

Cristiano Ronaldo amevunja rekodi ya dunia kwa kufunga magoli mengi katika soka ya kimataifa miongoni mwa wachezaji wa kiume baada ya kufiki bao lake la 110 na magoli 111 akiichezea Ureno katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Jamuhuri ya Ireland katika mchuano wa kufuzu kwa Kombe la dunia.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 alifunga magoli mawili kunako dakika za mwisho za mchezo-na hivyo kuvunja rekodi na kuipita baada ya kupiga mkwaju wa penalti uliyookolewa na Gavin Bazunu.

Ali Daei, ambaye aliifungia Iran mabao 109 kati ya mwaka 1993 na 2006, alishikilia rekodi sawa na ya Ronaldo huku akiiongeza mara dufu dhidi ya Ufaransa katika michuano ya Euro 2020

Mshambuliaji huyo wa Manchester United pia ameshikilia rekodi sawa na rekodi ya Ulaya ya Sergio Ramos upande wa wanaume- kwa kucheza mchezo wa 180 katika timu ya Ureno.

Rekodi ya dunia - iliyoridhiwa na Fifa msimu huu wa kiangazi- ni ya mataji 195 ya Malaysia ambayo aliyashinda Soh Chin Ann kati ya mwaka 1969 na 1984.

Ronaldo, ambaye alijiunga na Manchester United kutoka Juventus msimu huu katika siku ya mwisho , na , Daei ni wachezaji pekee wa kiume kuwahi kufunga mabao 90 au magoli mengi ya kimataifa.

"Ninafuraha sana, sio kwasababu nimevunja rekodi, bali kwa muda wa maalum ambao tulikuwa nao," aliiimbia RTE. "Magoli mawili katika mwisho wa mchezo. Ninapaswa kushukuru kile ambacho timu ilifanya . Tulikuw ana imani mpaka mwisho. Nimefurahi sana."

Hili ni tukio la kihistoria la hivi karibuni linaloidhinisha madai kuwa Ureno inapaswa kuchukuliwa kama timu bora ya nyakati zote.

Tayari ni mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika shindano kubwa zaidi la soka la klabu, Kombe la Ulaya/Championi Ligi, kombe ambalo amelishinda mara tano.

Ronaldo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid pia ni mchezaji aliyefunga mabao zaidi katika historia ya Mashindano ya Ulaya(14) na katika Euro na makombe ya dunia kwa pamoja (21).

Takriban nusu ya magoli aliyoyafunga Ronaldo aliyafunga katika dakika 30 za mwisho za mchezo.

Ametikisa nyavu mara 33 katika dakika z15 za mwisho za mchezo-mkiwemo mara mbili dhidi ya Irelnd-na mara 22 kati ya dakika ya 61 na dakika tya 75 ya mchezo .

Ronaldo amefunga magoli mara 17 kati ya dakika ya 16 na 30 na mara 16 kati ya dakika 31 na 45, na mara 11 katika dakika ya 15 zya kipindi cha kwanza na mara 12 katika dakika 15 za kipindi cha pili cha mchezo.

Baadhi ya magoli yake 91 ameyafunga ndani ya boksi huku 20 akiyafunga kutoka nje ya boksi. Amefunga mabao 14 kwa mikwaju ya penati na magoli tisa ameyafunga kwa mikwa ya moja kwa moja.

Lithuania na Sweden -saba kila moja - ni timu ambazo amezifunga zaidi alipocheza dhidi yake . Hakuwahi kuunga dhidi ya Jamuhuri ya Ireland kabla ya mchezo wa Algarve.

Jinsi Ronaldo ilivyovunja rekodi

Hakuna rekodi ya data rasmi kwa ajili ya washindi zaidi wa kimataifa wa magoli wanaume jambo linalofanya kuwa vigumu kusema ni nani anawekwa hasa kwenye safu ya wapi.

Ronaldo yuko juu kwa magoli 111 na Daei anafuatia kwa magoli 109, kwa hilo hapana shaka.

Daei wa Iran , aliyeichezea klabu ya Bayern Munich, anasemekana alivunja rekodi ya magoli ya Mhangary Ferenc Puskas mwaka 2003 kwa kufunga goli la kimataifa la 85. Huo ndio mwaka ambapo Ronaldo alicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa.

Kuna wanaoweza kudai kuwa magoli ya Daei yalifungwa dhidi ya upinzai rahisi-kwa kufunga magoli 95 dhidi ya klabu za upande wake za Asia.

Alifunga dhidi ya Maldives na Laos na sita dhidi ya ebanon.

Lakini Ronaldo amenufaika kwa kukabiliana timu dhaifu yakiwemo mabao sita dhidi ya Andorra na Luxembourg kila moja.

Swali pekee ni nani anayepanga safu chini yao? Mokhtar Dahari wa Malaysia - aliyecheza soka katika miaka ya 1970 na 80 - anasifiwa kama mchezaji aliyekuwa wa tatu katika baadhi ya maeneo akiwa na magoli 89. FIFA ilituma ujumbe wa Twitter msimu huu kuthibitisha hilo, licha ya kwamba haikuthibitishwa rasmi.

Puskas bila shaka ndiye anayefuata, akiwa na magoli 84 katika mataji 85 kwa ajili ya Hungary. Alikuwa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi Ulaya kabla ya Ronaldo.

Mchezaji wa Zambia Godfrey Chitalu alifunga mabao 79 kati ya miaka ya 1960 na 1980s -pia hayakuidhinishwa lakini pia alitajwa katika ujumbe huo wa Twitter wa Fifa.

Ronaldo huenda alivunje rekodi ya dunia, kama wachezaji soka wanawake , mshambuliaji wa Canada Christine Sinclair. Amefunga magoli 187 katika mechi 304 na bado hajastaafu.

Ronaldo apata moja juu ya Messi

Katika maajabu ya dunia ya sasa ya mashabiki wa Ronaldo na Lionel Messi, hii ni alama nyingine ya ushindi kwa Ronaldo.

Magoli 111 ya Ronaldo katika michezo 180 wazi vyema kwa magoli 76 ya Messi aliyoyafunga katika michezo 151 - kwa mahesabu ya haraka ni kama magoli 0.6 kwa mchezo ukilinganisha na 0.5.

Messi - ambaye ni mchezaji wa nane aliyefunga magoli zaidi duniani -ana umri w miaka 34 na kwa jinsi alivyo atahitaji kucheza hadi afike miaka 40 na zaidi ili kushinda magoli 111 ya kimataifa.

Ronaldo ameweka historia kimataifa katika soka

Ushindi utakaokumbukwa wa Ronaldo katika kazi yake kimtaifa bila shaka ulikuwa ni ushindi wa Euro 2016, ingawa alijeruhiwa mwanzoni mwa fainali.

Amesshinda magoli katika nusu fainali mbili za euro pia, kwa kipindi cha baada ya miaka 12-dhidi ya uholanzi katika mwaka 2004 na Wales mwaka 2016.

Muda wake bora zaidi katika Kombe la Dunia ulikuwa ni pale alipofunga mabao matatu kwa mpigo dhidi ya Uhispania katika ngazi za makundi miaka mitatu iliyopita nchini Urusi, ikiwa ni pamoja na mkwaju waq moja kwa moja . Hiyo ilikuwa ni moja ya ushindi wake wa tisa wa mabao matatu kwa mpigo katika mechi za kimataifa -ikiwa ni pamoja na moja dhidi ya Uholanzi Thkatika michuano ya nusu fainali ya Kombe la uefa la mataifa la mwaka 2019.l

Pia amefunga katika mashindano yote tisa makuu aliyowahi kucheza- Makombe ya dunia na Mahindano ya Uropa. Ikiwa ni pamoja na Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mataifa, ameshinda ndani mabao 11 kati ya 11.

Alishinda taji la Kiatu cha dhahabu katika Euro 2020 akifunga mabao matano katika michezo minne, akimpiku Mczech Patrick Schick aliyefunga mabao matano baada ya kupewa pasi na mchezaji mwenzake.