Beki David Luiz ajiunga na Flamengo baada ya kuondoka Arsenal

Atavalia jezi nambari 23

Muhtasari

•Mchezaji huyo ambaye aliondoka Arsenal na kuwa ajenti huru baada ya mkataba wake kuisha mwezi wa Julai ametia saini mkataba  utakaotamatika mwezi Desemba mwaka ujao.

Image: TWITTER// FLAMENGO

Beki David Luiz amejiunga rasmi na klabu ya Flamengo nchini Brazil.

Mchezaji huyo ambaye aliondoka Arsenal na kuwa ajenti huru baada ya mkataba wake kuisha mwezi wa Julai ametia saini mkataba  utakaotamatika mwezi Desemba mwaka ujao.

Luiz, 34 ambaye amechezea timu ya taifa ya Brazil katika mechi 57 atavalia jezi nambari 23 akichezea mabingwa hao mara saba wa ligi ya Brazil. Hiyo ndiyo ilikuwa nambari ya jezi yake akiwa Arsenal.

Hapo awali Luiz amechezea klabu tajika kama Benfica, PSG, Chelsea na hivi karibuni Arsenal.