Matokeo ya siku ya pili ya Champions League 2021/22

Muhtasari

•Timu zote ambazo zilihitimu kucheza kwenye UCL msimu wa 2021/22 sasa zimeshiriki kwenye mechi moja kila mmoja.

•Kwa sasa Man City inaongoza kundi A, Liverpool kundi B, Ajax wako kileleni katika kundi C, kundi D linaongozwa na Sheriff Tiraspol, Bayern inaongoza kundi E, Young Boys wako kileleni katika kundi F , Salzburg kundi G huku Juventus wakiongoza kundi H.

Image: TWITTER// MANCHESTER CITY

Mashindano ya Ligi ya Mabingwa (UCL) yameshika kasi huku mechi nane zaidi zikichezwa usiku wa Jumatano.

Timu zote ambazo zilihitimu kucheza kwenye UCL msimu wa 2021/22 sasa zimeshiriki kwenye mechi moja kila mmoja.

Michuano ya siku ya pili yalianza na mechi kati ya Besiktas na Borrusia Dortmund na Sheriff Tiraspol wakicheza dhidi ya Shaktar Donetsk mida ya saa mbili kasorobo.

Besiktas walipoteza 1-2 nyumbani dhidi ya Dortmund ilhali Tiraspol ya Moldova ikipata ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Donetsk.

Mechi zingine sita zilichezwa mida ya saa nne unusu.

Washindi wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) msimu uliopita Manchester City walipata ushindi mkubwa wa 6-3 dhidi ya wageni wake RB  Leipzig ya Ujerumani. Nathaniel Ake, Riyad Mahrez, Jack Grealish, Joao Cancelo na Gabriel Jesus wote walifungia City bao moja kila mmoja huku mabao matatu ya Leipzig yote yakifungwa na mshambulizi Christopher Nkunku.

Miamba wa soka Uhispania Real Madrid walishinda washindi wa Serie A ya Italia msimu uliopita Inter Milan bao moja kwa sufuri wakiwa ugenini.

Liverpool walicharaza AC Milan 3-2 ugani Anfield, mabao ya Liverpool yakifungwa na Mo Salah, Jodan Henderson na moja lilikuwa bao la kujifunga. Ante Rebic na Brahim Diaz walifungia AC Milan.

Ajax walipata ushindi mkubwa wa 5-1  dhidi ya wenyeji wao Sporting Lisbon huku mechi kati ya Club Brugge KV na FC Porto ikiishia sare ya 1-1.

Kwa sasa Man City inaongoza kundi A, Liverpool kundi B, Ajax wako kileleni katika kundi C, kundi D linaongozwa na Sheriff Tiraspol, Bayern inaongoza kundi E, Young Boys wako kileleni katika kundi F , Salzburg kundi G huku Juventus wakiongoza kundi H.